Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Afisa Mtendaji asema tutahakikisha tunawakamata wazazi ambao wanashindwa kuwatimizia mahitaji ya msingi ya watoto wao ikiwemo sare za shule.


Wanafunzi katika shule ya msingi Kagera Kata ya Ikunguigazi Mkoani Geita Wamepata changamoto kuhusu  Sare za shule kwao jambo linaloshusha ufanisi wa  kitaaluma pindi wanapokuwa darasani.
  
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Nd. Mahebe Chigulu amesema Watoto ambao hawana sare za shule hususani viatu wanakuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa wanapoenda msalani pasipo kuvaa viatu.
Hata hivyo amefafanua kuhusu  kisaikolojia watoto ambao hawana Sare timilifu wanaathirika, kwani kunabaadhi ya wanafunzi wanatabia ya kunyanya paa wenzao.

 Kwa baadhi ya  wazazi wamesema hali ngumu ya maisha,migongano katika familia pamoja na matumizi mabaya ya pesa kwa baadhi ya wazazi vimekuwa ni sababu kuu za wao kushindwa kuwanunulia sare za shule watoto wao.
  
  Afisa mtendaji wa kijiji cha Kagera amesema watahakikisha wanawakamata wazazi ambao wanashindwa kuwatimizia mahitaji ya msingi ya watoto wao ikiwemo sare za shule na ameitaka jamii kushiriki kwa pamoja katika kuwanunulia sare za shule.
NA NICKORAUS PAUL LYANKANKANDO GEITA.

Post a Comment

0 Comments