Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Hakikisheni mnawachukulia hatua watuhumiwa ambao walitoroka baada ya kuwafanyia vitendo vya ukatiri wa Watoto ili iwe fundisho kwa watu wengine.


   Akizungumza baada ya semina ya kutetea na kupinga ukatiri wa kijinsia kwa makundi yasiyojiweza iliyofanyika katika halimashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani kagera Mkurugenzi msaidizi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria hapa nchini Bi. Felicia Joseph amesema kuwa hadi sasa Wizara hiyo imeishasajiri mashirika yanayotoa msaada wa kisheria zaidi ya 90 pamoja na wasaidizi wa kisheria zaidi ya 400 hivyo inatakiwa kutoa haki na kujiepusha vitendo vya Rushwa.

   Naye Mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa mashirika yanayotoa msaada  wa kisheria hapa nchini  Bi.Kristina Ruhinda amesema hadi sasa kwa Mkoa wa Kagera wameweza kuwafikia wananchi zaidi ya laki moja kwani wamejipanga kulinda na kuondoa unyanyasaji wa kijinsia kwa Watoto hasa Mtoto wa kike ikiwemo kutoa elimu mashuleni   kwa kushirikiana na serikali.

   Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa kagera Brigedia jenerali Marko Gaguti Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo kuhakikisha wanawachukulia hatua watuhumiwa ambao walitoroka baada ya kuwafanyia vitendo vya ukatiri wa Watoto ili iwe fundisho kwa watu wengine.

   Nao baadhi ya wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Kagera wakiwemo maafisa ustawi wa jamii Bi Rosemary Nicodemas ,Japhert Kanoni na Denis Daniel wamesema kuwa changamoto kubwa wanazokumbana nazo katika kukomesha vitendo hivyo katika jamii ni pamoja na kukosa ushirikiano kutoka kwa waanga wa vitendo hivyo wakiwemo wazazi wa Watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia Pale kesi inapokuwa mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua watuhumiwa.
Post a Comment

0 Comments