Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Je,mpango wa Wizara ya Afya kuunda vikundi vya malezi ili kukomesha ukatili kwa watoto utazaa matunda?

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imewezesha uanzishwaji wa vikundi vya malezi katika Kata mbili za Halmashauri ya Mji wa Nzega mkoani Tabora.
   Akizungumza katika Kata ya Nzega Magharibi Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima amesema lengo la kuanzishwa kwa vikundi vya malezi katika jamii ni kuisaidia jamii kupata elimu sahihi ya malezi ili kuondokana na vitendo vya kikatili.
  
  Hata hivyo Bi. Tausi amesema kuwa jamii inawajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wanapata malezi bora ambayo yatamuweka mbali na vitendo vya ukatili ambapo kwa sehemu kubwa vimekuwa vikiwaharibu watoto hasa kisaikolojia.
  Ameongeza kuwa Serikali katika kuhakikisha vikundi hivyo vinapata nguvu ya kutekeleza wajibu wao imekuja na Kitini cha Malezi ya Familia ambacho kitawasaidia kupata nyenzo muhimu za namna ya kuwapa malezi bora Watoto katika jamii.

  Bi. Tausi amesisitiza kuwa vikundi vya malezi vitasimama vizuri basi watoto wetu watapata malezi bora na kuwezesha kuwa na taifa lenye kuwajibika katika kuwajenga watoto katika malezi.
"Vitendo vingi vya ukatili kwa Wat's katika vinafanywa na wazazi/walezi na watu wa karibu hivyo tunahitaji elimu ya malezi ili kuhakikisha knatokomeza vitendo hivi" alisema Bi. Tausi
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Halmshauri ya Mji wa Nzega Bi. Mwajuma Kisoma amesema kuwa vikundi vya malezi ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha watoto wanapatiwa malezi bora ambayo yatasaidia kuondokana na vitendo vya ukatili katika jamii.
 Taarifa hii nikwa mjibu wa  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.

Post a Comment

0 Comments