Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

NENDA UKAANDIKE MAJIBU YA UONGO ILIUSIFAURU MITIHANI NIKWABAADHI YA WAZAZI MKOANI TABORA, SERIKALI IMEAHIDI KUCHUKUA HATUA DHIDI YAO.


Wazazi na walezi katika tarafa ya IGAGALA wilaya ya KALIUA mkoani TABORA wametakiwa kuacha tabia ya kuwaambia watoto wakaandike majibu ya uongo kwenye mitihani ili wasifaulu.
Rai hiyo imetolewa na afisa tarafa wa IGAGALA, SIMON MALANDO kwenye mahafari ya 38 katika shule ya msingi KAMSEKWA ambapo amesema wapo baadhi ya wazazi wamekuwa wakitoa ushawishi kwa wahitimu kuandika majibu ya uongo huku akiongeza kwa kusema serikali itachukua hatua kwa watakaobainika.

  SALUM YUSUF ni mkazi wa kata ya KAMSEKWA ameiomba serikali kuchukua hatua kwa wazazi na wanafunzi wanaobainika kuandika majibu ya uongo kwenye mitihani.
Jumla ya wanafunzi 70 wanataraji kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba katika shule ya msingi KAMSEKWA kati yao wasichana ni 33. NA  Simon Jumanne KUTOKA KALIUA.

Post a Comment

0 Comments