Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Sina fuvu kisogoni kwangu isipokua Ngozi na nywere tu,Maji maji ndio yalio jaa kisogoni, naomba msaada wa kifedha kwa wa Tanzania iliniendelee kupata matibabu nipone niendele na masomo.

   Mtoto mwenye umri wa miaka kumi na mbili (12) jina lake limehifadhiwa , anaeishi na Baba yake mzazi katika mji mdogo wa Ifakara uliopo Mkoani Morogoro, tangu kuzaliwa kwake amekuwa na Uvimbe kwenye kichwa chake ulio sababisha kichwa kujaa maji eneo lote lakisogo kichwani kwake, natatizo hilo liligundulika miaka mitatu badae (3) baada ya kinyozi wa saluni kupitisha mashine yake na kugundua sehemu ya kichogo cha Mtoto huyo sio kigumu kama wengine isipokuwa ninywere na ngozi ndivyo vilivyo ziba na kuziba aendelee kuwa hai mpaka sasa.
    
   TKT Radio ilifanikiwa kukutana na familia , Baba yake ambae ni Sabas Mapande Yeye ni mkulima anahangaika  kutafuta pesa kwa shughuli zake za kilimo ilimradi tu, Mtoto apate matibabu hospitali ya Taifa Muhimbili, ambako anatibiwa tangu ugonjwa huo ulipobainika, na baada ya kubainika ungonjwa huo mwaka mmoja baadae Mama mzazi wa Mtoto huyo akaachana na Baba mzazi wa mtoto na kwenda kuolewa na mwana ume mwingine hadi sasa.
  
    Aidha Inatakiwa laki tisa (Tsh,900,000/=) kila baada ya miezi mitatu,hii nikwaajili ya Matibabu,Chakula,Usafiri na kulipia chumba chakulala kwasiku zote wazokuwa  wameambiwa na Daktari kusubiri wakiwa Jijini Dar es Salaam,Ndg. Mapande amelejea kwa watanzania ilikuona mwenye uwezekano wakumsaidia kumnunulia Mashine ya kumwagiria kwaajili ya bustani ambao ndio utakuwa mtaji mkubwa kwake , ilianze kilimo hicho kwani shamba analo lililoko bondeni na lina maji yakutosha shabaa yake ikiwa kusitisha kuomba omba pesa kwa watu ilikumtibia mwanae.
   
    Hata hivyo Mapande  amesema  kufikia mwezi December  inatakiwa  zaidi ya Mlioni moja na nusu (1500,000/=) kwaajiri ya kununua kipande cha Fuvu la badia ilikumuekea eneo lote la kisogo ambalo liko wazi, Na TKT Radio ili mtafuta Daktari wa magonjwa  ya Ubongo ilikufahamu Sababu zinazo sababisha kutokea kwa  Ugonjwa huo kwa Watoto wadogo, ilishindikana kutokana na kuwa na Ratiba ngumu ya kikazi tutakapo mpata tuta chapisha majibu yake hapa.
  Tafadhali wasiliana na Baba wa Mtoto huyo ambae ni Sabas Mapande
                                   Sabas Mapande +255684585251.Post a Comment

0 Comments