Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Tunaomba wasamalia wema waje kuwajengea choo watoto hawa wenye mahitaji maalumu,bi, Mkonongo kutoka mkoani Songwe.Walimu wa kitengo cha Watoto wenyemahitajimaalumu, kilichopo katika shule ya msingi Mlowo mkoani Songwe waiombaserikali, wadau na Mashirika mbalimbali kusaidiakituohicho kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kituonihapo.
  Akizungumza na Tkt Radio Mkoani humo Mkuuwakitengo hicho Mwalimu Judith Mkonongo amesema kituo hicho kinachangamoto nyingi hususani Madarasa na Vyoo sirafiki kwa Watoto walio na mahitaji kama waliopo kituoni hapo.
  Hata hivyo Bi, Mkonongo amewaomba wasamalia wema kufika shuleni hapo wawatembelee Watoto hao ilikuawatia moyo,  mbali na hivyo watakapo fika hapo shuleni wanaweza kuchangia ujenzi wa madarasa ambayo nirafiki kwao pamoja na vyoo.
  Aidha Mwl.Kenedy  Msokile yeye nimwalimu wa wa taaluma  katika shule hiyo amesema changamoto wanazo kumbana nazo kwenye majukumu yao niukosefu wa vitendea kazi kama vile vifaa vya kupimia ilikubaini kiwango cha usikivu kwa Watoto wenye ulemavu wa masikio, Nukta Nundu kwa Watoto waio ona.
Na Mr.Hamidu kutoka Songwe.

Post a Comment

0 Comments