Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Kukamilika kituo cha afya zaidi ya mwaka mmoja sasa na bado hakuna wahudumu hakina msaada wowote hatakama kimejengwa hapa,Maana wakezetu wanaendelea kujifungulia vichakani,wakiwa njiani kufuata hudumahiyo.Ni Wilaya ya Geita Vijijini iliopo mkoani wa Geita.


  
 Kilio cha wananchi wa Kijiji cha Magenge  Wilaya ya Geita Vijijini, waendelea kuiomba serikali kuwaletea Wahudumu wa Afya kwenye zahanati ya kata yao maana wanatembea zaidi ya msaa  (5) kutoka kijijini kwao kwenda Katan nyingine.
    
   Wakizungumza na Tkt Radio Baadhi ya Wanawake Keflay Samweli nawengine kwasharti lakutotajwa majina yao Kijijini hapo, wamesema  adha wanazo kumbana nazo nikubwa hususani wakati muda unapofika wa mama kuhudhuria kiliniki ya ujauzito, Kupeleka Watoto kupata chanjo,Matibabu na Ushauri inakuwavigumu maana wanatembea zaidi ya kilometer 5 kufuata huduma hiyo katika Kata nyingine ambako huduma ya Mama na Mtoto hutolewa.
  
   Hatahivyo  Ndg. Nikodem Paul amesema Zahanati hiyo imeanza kujengwa tangu mwaka 1994 na imekamilika mwishoni mwa mwaka uliopita  wa serikali,lakini wahudumu hawajaletwa kwaajili ya kuwahudumia wananchi, Jambo linalosababisha Mama wajawazito kujifungulia vichakani kutokana na kutembea muda mrefu kufuata huduma ya Zahanati. Kwa upande wa uongozi wa serikali kwa ngazi ya Mwenyekiti wa Kijiji Ndg.Tano Manamba amewaomba wananchi kuendelea kuvumilia maana serikali inakumbuka jambo la Zahanati hiyo.
 

Post a Comment

0 Comments