Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MAMA AMBAKA MTOTO WA KIUME MIAKA (9) WA JIRANI YAKE GAIRO MKOANI MOROGORO.Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Shani Chamwela (35), mkazi wa Magoeko wilayani Gairo, anakabiriwa na kesi ya  kumrubuni na kumbaka mtoto wa kiume ambaye niwajirani yake tangu akiwa na umri wa miaka tisa hadi mwaka huu ikiwa anaumri wa miaka kumi na miwili.


Kesi hiyo No.65/ ya mwaka 2019 ilifunguliwa tarehe  13/01/2019 katika wilaya ya Gairo na baadae  ilihamishiwa Wilaya ya Kilosa, kutokana na uzito wa kesi hiyo illiamriwa isikilizwe katika Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro ikiwa tarehe 18 Machi mwaka huu,  ilisikilizwa kwa Mara ya Kwanza katika mahakama hiyo na Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo Bi. Elizabeth Nyembele.

Aidha mshtakiwa huyo Shani Chamwela alikana kumfanyia ukatili huo kupitia kwa wakili wake John Kidandu ambaye anasimamia kesi hiyo, na kueleza kwamba familia ya mtoto huyo inamsingizia, hivyo ameiomba mahakama kuletwa kwa ushahidi wa picha au video inayoonesha mteja wake akifanya kitendo hicho.

Alipohojiwa mtoto huyo na mahakama  alisema amechoshwa na kitendo hicho cha mama huyo kwani ni miaka minne Sasa tangu anze kumlazimisha kufanya kitendo hicho, pia amekuwa akimtishia kumuua endapo angesema kwa watu Jambo  hilo.

Hadi Sasa kesi hiyo imefikisha miezi kumi tangu kufunguliwa huku Mama na Bibi wa mtoto huyo waliiomba Mahakama kutoipaleka kutoisogeza mbali katika  tarehe inayotajwa kwani inaathiri masomo ya mtoto huyo ambaye sasa anasoma darasa la sita Kila wanapohudhuria Mahakamani.

Kesi hiyo No.65 inasimamiwa na mawakili wawili kwa upande wa serikali Edger Bantulaki na Theodora Mlelwa baada ya kusikilizwa mashahidi wawili wa upande wa mlalamikaji imeahirishwa Hadi tarehe 08 Novemba mwaka huu itakaposikilizwa tena.

Post a Comment

0 Comments