Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Msiba wa maji si kwenu tu hata hukunako ,Wanafunzi wa shule ya sekondari Ikunguigazi Wilaya ya Mbogwe Mkoani wa Geita wazungumza.   Wanafunzi wa shule ya sekondari  Ikunguigazi Wilaya Mbogwe Mkoa wa Geita wameiomba serikali kuwachimbia visima vya maji safi na salama kutokana na umbali wa huduma hiyo inapo patikana, Ambapo inawagharimu zaidi ya saa moja kutafuta maji hadi kuyapata na kusababisha kuisha wa  vipindi darasani.
Wakizungumza na Tkt radio wanafunzi hao wamesema maji hayo wanayofata nikutoka katika visima vya kijiji cha kagera pamoja na madimbwi hali ambayo inahatarisha afya zao kutokana na maji hayo kuyatumia kunywa pamoja na kupikia na wameiomba serikali kusikia kilio chao.
  
    Mwalimu mkuu wa shule hiyo ndg.Stephano Kusana,Amesema wao kama shule walifanya jitihada za kutatua tatizo la maji Kwa kufanya harambee ya changizo lakini ilishindikana kutokana na uzito wa tatizo hilo na Ameiomba serikali isilifumbie macho.

   Afisa mtendaji wa kata hiyo ndg Renatus Mwakalembe, yeye kwa kujibu malalamiko ya ukosefu wa visima vya maji shuleni hapo,Amesema changamoto ya maji katika shule hiyo anaitambua upo mkakati wa Kuongeza urefu wa kisima ambacho kilishindwa kukamilika kutokana na waliopewa kandarasi hiyo kukimbia nakushindwa kukamilika jambo linalosababisha ugumu wa kupata huduma hiyo shuleni hapo.

   Mbali na changamoto hiyo ya maji shule hiyo inachangamoto ya umeme kwani wanatumia umeme wa sola lakini hayo hayakuwafanya walimu kukata tama pamoja na wafunzi wao,katika mtihani wa mocko mkoa shule hiyo ilishika nafasi ya kwanza kwa ngazi ya kikata na Wilaya ya Mbogwe.
                        Na Nichoraus Paul Lyankando, Mbogwe Geita.

Post a Comment

1 Comments