Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ndoto zetu nikuwa wahasibu na madaktari,nimaneno ya wanafunzi kutoka shule ya msingi kinole katika kijiji cha kinole kilichopo wilaya ya Morogoro vijijini.


Watoto wana mengi ya kusema endapo tu, utaweka mazingira ya kuwasikiliza nini walicho nacho kwenye mawazo yao na malengo yao,  hayo yamebainika baada ya  TKT/UN Radio kutembelea shule ya msingi Kinole iliopo kijiji cha Kinole huko Morogoro vijijini katika Mkoa wa Morogoro.
Aidha Aslatha Hmisi yeye ameeleza malengo yake kwenye maisha anataka kuwa muhasibu , hivyo inampasa kusoma sana masomo ya hisabati na masomo mengine ya sayansi,  na Hamisa Twaa huyu ni dada mkuu wa shule ya msingi Kinole anasoma darasa la sita b amebainisha kwamba hapendi kuona watoto wenzake wana nyanyaswa hasa wanao fanya kazi za ndani.

  Hata hivyo Mtoto Hamisa ndoto zake nikuwa daktari wa kutibu binadamu ilikushirikiana na madaktari waliopo kwa sasa na atakaowakuta kipindi hicho, kwa upande mwingine Chief Kingalu wakabila la waluguru mkoa wa Morogoro amewaomba wananchi wake kuongeza staha na bidii kwenye kazi zao za kuwaingizia kipato ilikumudu kuwasomesha watoto wao hadi elimu ya juu ikiwa ni moja ya njia bora ya kutimiza ndoto za watoto wao.

  Kwaupande wa wazazi Pendo Sanga na Sophia Hassani wakazi wa kijiji cha Kinole wamesema kwabaadhi ya familia zingine zina maisha magumu zaidi japo kazi za kuwaingizia kipato kwa waliowengi nikilimo, inafika wkati  wengine wanashindwa kumsomesha mtoto kwa kiwango cha ellimu ya juu hata vyuo vya ufundi kwa ukosefu wa pesa za kutosha.Hivyo nibora mashirika kwa kushirikiana na serikali kulepeleka elimu ya kilimo biashara ilikuondokana na kilimo mazoea vijijini jambo hilo litaongeza kipato kwa familia nyingi nakuendelea kutimiza ndoto walizo nazo watoto wao.

Post a Comment

0 Comments