Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ufumbuzi wa patikana kwa Mama wajawazito katika wilaya ya KALIUA mkoani TABORA baada ya chumba cha upasuaji kuanza kutoa huduma.
   Ufumbuzi wa patikana kwa Mama wajawazito katika wilaya ya KALIUA mkoani TABORA baada ya chumba cha upasuaji kuanza kutoa huduma.
   
   Rai hiyo imetolewa na kaimu mganga mkuu wa wilaya ya KALIUA, Daktari CHARLES CONRAD kwa kusema kukamilika kwa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya KALIUA kumesaidia kupunguza vifo vya mama au mtoto nakuongeza kwa kusema tangu kwa huduma ya upasuaji ianze kutolewa jumla ya kinamama 120 wamepata huduma ya upasuaji huku akitoa mwito kwa kinamama kufika kupata huduma sasa.
  
   ALIKUSHUBILA RICHARD ni muuguzi mkuu katika kituo cha afya KALIUA  ameiomba serikali kuongeza watumishi ili kuendelea kutoa huduma iliyo bora. Hata hivyo mmoja wa kinamama TABU DAMALALA amepongeza huduma inayotolewa katika kituo hicho cha afya hasa ya upasuaji.
  
   Akizungumzia upungufu wa watumishi wa afya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya KALIUA, Daktari JOHN PIMA amesema serikali imeleta watumishi watatu (3) wa idara ya afya huku akibainisha hatua ambazo halmashauri inafanya ili kupunguza uhaba wa watumishi wa afya, Aidha ameongeza kua serikali ya awamu ya tano ni sikivu hivyo anaimani itaendelea kutatua changamoto ikiwemo kuongeza watumishi wa afya.   
          Na Simon Jumanne Kaliua Tabora.

Post a Comment

0 Comments