Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo kwa baadhi ya maeneo hapanchini bado ni changamoto.  Shule ya msingi Kamsekwa katika wilaya ya Kaliua mkoani Tabora inakabiliwa na upungufu wa vyumba kumi na nne (14) vya madarasa huku ikiwa na jumla ya wanafunzi elfu moja na  kumi na moja (1,011).
  
  Akizungumza na Tkt Radio mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kamsekwa, Fabiani Masanja amesema kutokana na upungufu wa madarasa imekuwa ikiwalazimu darasa moja kuwa na wanafunzi zaidi ya mia moja hivyo kufanya ufundishaji kuwa mgumu,wakati huo nyumba za waalimu na matundu ya vyoo shuleni akitaja kuwa nitatizo lingine lililopo shuleni hapo.
  
  Nao baadhi ya wanafunzi wameiomba serikali kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwa ndionjia pekee na chachu ya kupandisha kiwango cha taaluma shuleni hapo,jambo lingine linalo wasumbua nikujazana kwenye chumba cha darasa jambo linalo sababisha ongezeko la joto kutokana na wingi wa wanafunzi.
Joseph Bilasa ni afisa mtendaji wa kijiji cha Kamsekwa ameweka wazi mikakati ya kuboresha miundombinu shuleni hapo, amesema kuanzia mwezi ujao atahitisha kikao cha wazazi ili kukubaliana kuanza kuchimba mashimo ya choo,hiyo ikiwa nihatua ya kuboresha miundo mbinu ya shule hiyo.

  Nae afisa tarafa ya Igagala, Simon Malando amewataka wananchi kushirikiana na serikali kutatua changamoto za shule kwani jambo hilo nifaida kwa jamii nzima sio jambo la kuiachia serikali,Wazazi wanatakiwa kuendelea kuwa andikisha watoto shule na kuendelea kuwahimiza kuongeza jitihada za kusoma ilikutimiza ndoto zao.

         Na Simon Jumanne kutoka Wilaya Ya Kaliua Mkoani Tabora.

Post a Comment

0 Comments