Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Kesi ya ubakaji kwa mtoto mdogo no.65 ya mwaka 2019 inayo mkabiri shani chamwela (35) inayosikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa morogoro imeahirishwa hadi tarehe 11/12/2019 itakapo sikilizwa tena. Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Shani Chamwela (35), mkazi wa Magoeko wilayani Gairo, anaekabiriwa na kesi ya  kumrubuni na kumbaka mtoto wa kiume ambaye niwajirani yake tangu akiwa na umri wa miaka tisa hadi mwaka huu ikiwa anaumri wa miaka kumi na miwili.

  Kesi hiyo No.65/ ya mwaka 2019 ilifunguliwa tarehe  13/01/2019 katika wilaya ya Gairo na baadae  ilihamishiwa Wilaya ya Kilosa, kutokana na uzito wa kesi hiyo illiamriwa isikilizwe katika Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro ikiwa tarehe 18 Machi mwaka huu,  ilisikilizwa kwa Mara ya Kwanza katika mahakama hiyo na Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo Bi. Elizabeth Nyembele.

 Hata hivyo ilitakiwa kusikilizwa tarehe nane 08/11/2019 imeahirishwa baada ya hakimu aliepaswa kuisikiliza hakuwepo na badala yake imepangwa kusikilizwa tarehe 11/12/2019 katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro.

Post a Comment

0 Comments