Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Miaka 30 tangu kupitishwa kwa mkataba wa haiki za mtoto,Mama wa kambo mnao olewa na baba zetu baada ya mama zetu kufariki au kuachana mtupende pia sisi watoto mliotukuta,Nasio kutufanyia ukatili nakuonekana hatufai tena kwa baba zetu.


Siku ya Mtoto Duniani wahusika watoa maoni mbalimbali.


                                                                              
Mkataba wa wa kimataifa wa Haki za Mtoto ulipitishwa tangu Novermber 20,1989 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York , Ambapo Tanzania ni mwanachama wa mkataba huo na leo ikiwa ni November 20,2019 umetimiza miaka 30 tangu kupitishwa kwa nchi wa nachama.
 Shirika la kuhudumia Watoto duniani nchini Tanzania UNICEF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto wameadhimisha siku hii katika ukumbi wa  mikutano  ya kimataifa wa Julius Nyerere uliopo Mjini Dar es salaam.
 Aidha Tanzania kama ilivyo Nchi nyingine Wanachama ilitia saini mkataba huu tarehe 1 Juni, 1990 na kuuridhia tarehe 10 Juni, 1991 ambapo siku hii imetengwa mahususi kuikumbusha Dunia kuwa, watoto wana haki ambazo hazistahili kupuuzwa. Hata hivyo kuna idadi kubwa ya watoto Duniani wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukiukwaji mkubwa wa haki za Mtoto na ukatili wa aina mbalimbali kama vipigo, kubakwa, mimba na ndoa za utotoni, ukeketaji, ulawiti, vitisho, umasikini unaowanyima mahitaji ya msingi, utumikishwaji, kuhusishwa na vita vinavyopelekea ulemavu na hata kupoteza maisha. Hivyo, lengo la kuadhimisha siku hii ni kuelimishana na kuikumbusha jamii nzima ya watanzania hasa wazazi na walezi wajibu wao katika kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi.
 Hata hivyo mkoani Morogoro TKT Radio imezungumza na  Watoto kutoka shule mbali mbali wametoa maoni yao kuhusu mkataba wa Haki za Mtoto ambapo John Moris yeye amesema Mkataba huu unawasaidia Watoto kuwalinda katika ukatili wanao fanyiwa, huku Jackson Teobadi yeye amewaasa wazazi wakambo kuwatunza watoto  wa wawa mama wengine bila kuwatesa kwani hao pia wanahaki ya kuishi kama watoto wake.
                                                                                   

Post a Comment

0 Comments