Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Mtoto alie bakwa noveber 9 mwaka huu aiomba serikali kumrinda kutokana na mke wa mtuhumiwa wa Ubakaji kutoa maneno ya vitisho kwa mtoto huyo,Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.


    
 Siku chache zimepita baada ya mtu mmoja alie julikana kwa jina la Benjamin Samweli mwenye umri wa miaka hamsini mkazi wa kijiji cha mwingilo Wilaya ya mbogwe kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka kumi na moja na  mpaka sasa anataftwa,ambapo mke wa mtuhumiwa huyo ameanza kumtolea maneno ya vitisho mtoto huyo kuhusu tukio lililo fanywa na mmewake.
  
  Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 11 anayesoma darasa la tatu katika shule  ya msingi Mwingilo alibakwa mnamo tarehe 9 novemba na mtuhumiwa huyo kutokomea kusiko julikana mpaka sasa, mtoto huyo ameiomba serikali imulinde kutokana na maneno ya vitisho vya mke wa pili wa mtuhumiwa huyo,Hatahivyo ameimba serikali ulinzi kwa maisha yake kutokana na vitisho anavyo vipata kutoka kwa miongoni mwa wake wa mtuhumiwa huyo.

  Kwa upande wao wazazi wa mtoto huyo wamesema baada ya kupata taarifa za mtoto wao kupewa vitisho na mke wa mtuhumiwa waliamua kutoa taarifa mapema kwenye ofisi ya sungu sungu ili mtoto wao awe salama,hata jambo lolote likitokea uongozi wa serikali uweunataarifa ya vitisho hivyo.

 Mke wa mtuhumiwa huyo ambaye ni mke Wa pili ameanza kumtolea maneno ya vitisho mtoto pindi anapokutana naye kijijini hapo, mama huyo anaamini kwamba Mtoto huyo alikuwa mke wa tatu wa mume wake,hivyo kutokana na umri wa mtoto huyo haulingani kuwa mke mwenza.
Aidha mtemi wa sungu sungu katika kijiji hicho ndg John Lusuga amesema alipata malalamiko hayo kutoka kwa wazazi wa mtoto huyo nakuwaahidi kuendelea kumlinda Mtoto huyo,kwani walipo pata taarifa kutoka kwa wazazi wa Mtoto huyo walimuita mke wa mtuhumiwa na kumuonya kuhusu kuendelea kutoa maneno ya vitisho kwa Mtoto huyo.
                                 
                            Na Nichoraus Lyankando Mbogwe Geita.  


Post a Comment

0 Comments