Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Takwimu ya wizara ya afya kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watoto nchini,kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inayo adhimishwa November 25 ya kila mwaka.


  Takwimu za Utafiti wa Hali ya Afya na Watu na Viashiria vya Malaria (TDHS-MIS 2015/2016) zinaonesha kuwa wasichana balehe 4 kati ya 10 wamefanyiwa ukatili wa kimwili, na asilimia 17 wamefanyiwa ukatili wa kingono kati ya umri wa miaka 15-19. Aidha, mtoto 1 kati ya 2 wa kike na kiume wa umri kati ya miaka 13-19 wamefanyiwa ukatili wa kimwili. Pia, mtoto 1 kati ya Watoto 10 wa kike amefanyiwa ukatili wa kingono na Mwalimu wake. Kadhalika, takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 27 ya wasichana wenye umri wa miaka 15-19 wamezaa; na asilimia 57 ya wanawake wa umri wa miaka 19 wameshakuwa na watoto ambapo wasichana 2 kati ya 5 wameolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
 Aidha, kwa mujibu wa Takwimu za Jeshi la Polisi nchini za mwaka 2017, zinaonyesha kuwa matukio 13,457 ya ukatili dhidi ya watoto yaliripotiwa katika vituo mbalimbali vya Polisi Nchini ukilinganisha na matukio 10,551 kwa mwaka 2016. Taarifa hiyo inaonyesha kuwa mikoa mitano (5) ya Kipolisi inayoongoza kwa kuwa na takwimu kubwa za ukatili ni Kinondoni (2,426), Dodoma (1,283), Tanga (1,064), Temeke (984) na Arusha (972).
 Ili kukabiliana na changamoto zilizoainisha dhidi ya Watoto wetu, Serikali imeandaa Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008; Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Jinsia ya mwaka 2001; Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014; Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 na Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 ambapo imeweka kipengele kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kusababisha mimba kwa mtoto wa shule na pia kumuoza na hatimaye kukatisha masomo atashitakiwa na akipatikana na hatia atatumikia kifungo cha hadi miaka 30 jela.

Post a Comment

0 Comments