Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Shirika lisilo la kiserika la The Same Qualities Foundation limerejesha furaha kwa zaidi ya Watoto 500 wenye ulemavu wa Midomo Sungura kwa kuwafanyia upasuaji midomo yao hapa nchini bure,kwamjibu wa taarifa ilio tolewa leo na mkurungenzi wa shirika hilo Dr.Peter Mabula jijini Arusha.Shirika lisilo la kiserika la The Same Qualities Foundation lenye makao makuu yake jijini Arusha, linatoa huduma za Kidaktari kwa kusaidia kwenye matukio ya dharura na watoto wenye ulemavu wa kuzaliwa nao kamavile Midomo Sungura, Vichwa Maji na Magonjwa mengine katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwafanyia upasuaji bure pasipo malipo yeyote, ilikurejesha furaha,usawa na kuzuia ubaguzi kwa walio na ulemavu huo kwenye jamii.
   
  Aidha akizungumza na Tanzania Kids Time kwa njia ya simu mkurungenzi wa Shirika hilo Dr. Peter Mabula ambae ni Daktari bingwa wa magonjwa ya dharura na ajali (Emergency Physician) amesema timu ya Madaktari bingwa kutoka kwenye shirika hilo watatoa huduma ya upasuaji kwa watoto walio na ulemavu wa Mdomo Sungura,ambapo zoezi hilo litafanyika December 16-20 mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na upasuaji huo utakuwa ni bure kabisa.
 
 Hatahivyo Dr.Mabula amebainisha kwamba Mpaka sasa wameshasaidia (upasuaji) kwa zaidi ya Watoto 500 kwa miaka mitano iliyopita,kwanishabaha yao nikuisaidia jamii katika familia zilizo na Watoto wenye ulemavu huo ili kuwarejeshea furaha katika familia hizo, mkurungezi huyo akatumia nafasi hiyo kuwa asa wazazi na walezi walio na watoto wenye ulemavu huo kuwafikisha kwenye ofisi zao ilikupangiwa tarehe ya kufanyiwa upasuaji kwani hakuna gharama yeyote atakayo lipa Mzazi au Mlezi kuhusu huduma hiyo.  

Post a Comment

0 Comments