Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ushindi wa Nuru Ally katika shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama MAVUNDE TALENT SEARCH 2019, waleta hamasa kubwa kwa wazazi huko jijini dodoma.


Wazazi  na walezi  nchini wamehimizwa  kuwaunga mkono watoto wao  pindi wanapoonyesha kuwa na vipaji kwa kuviendeleza badala ya kuvipuuza kwa kuwavunja moyo  ili waweze kutimiza ndoto zao  wakati wote wa masomo ya o na hata baada ya kuhitimu.
Hayo yamesemwa na evelina Mkwangala mkazi wa ipagala jijini Dodoma  ambaye ni mama mazazi wa mwanafunzi  wa shule ya msingi chadulu baada ya mtoto wake  kuibuka  kidedea  katika kipengele cha nyimbo  miongoni mwa vipengele mbalimbali ikiwemo, upigaji kinanda, ngoma, gitaa, mpira wa miguu na nyimbo kwenye mashindano ya kusaka  vipaji  kwa shule za msingini mkoani humo .

  Mashindano hayo ya kusaka vipaji yameandaliwa na mbunge wa Dodoma mjini mh. Anthony Mavunde  na kufanyika  Desemba 4 mwaka huu katika ukumbi wa Dear Mama  yakijulikana kama MAVUNDE TALENT SEARCH 2019 yakiwa na kauli mbiu ya DODOMA YANGU KIPAJI CHANGU yakilenga kuibua vipaji vya watoto na kuvikuza.
Akizungumza   na mwandishi wetu Mkwangala  alisema kuwa  wazazi wengi wamekuwa wakiwakazania watoto wao katika masomo ya darasani pekee na kusahau uwezo asilia wa watoto wao hali ambayo husababisha kufa kwa vipaji vyao kudidimia ambapo vingeendelezwa wangeweza kupiga hatua kubwa katika maisha yao.

  Wazazi wanapasawa kuwaruhusu watoto wao wenye vipaji kushiriki mashindano mbalimbali kuonyesha uwezo wao na kutambulika pamoja na kuwatia moyo kuliko kuwakataza kwa kudai kuwa watafeli masomo siyo kweli” alisema Mkwangala.
Kwa upande wake mwanafunzi  wa darasa la tano kutoka shule ya msingi chadulu aliyeibuka mshindi Nuru ally  alisema amepokea kwa furaha ushindi huo akisema kuwa siri ya mafanikio yake ni uwezo wake wa kuimba , kuzingatia maelekezo aliyokuwa akipewa wakati wote wa mashindano huku akiishukuru familia yake, walimu na wanafunzi wenzake kwa ushirikiano wao hadi kufikia hatua hiyo ya kuibuka mshindi na kuwakilisha shule yao licha ya  ushindani mkubwa uliokuwepo.

  Ningekuwa sijui kuimba ningeshindwa kwa sababu majaji walikuwa wanaangalia sauti siyo nyimbo natamani kuwa muimbaji bora huko baadaye niendelee kuishi kwenye ndoto zangu”. Alisema Nuru.
Naye mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini patrobasi katambi ambapo aliwataka viongozi wengine kuiga mfano huo katika maeneo yao hatua itakayowezesha kuwakuza watoto katika hali ya kujiamini na kusimamia uwezo wao .

  Aidha shule zilizoshinda tatu bora kwa kutoa  washindi 20 walioshinda katika vipengele hivyo  ni shule ya msingi CHADULU iliyoshika nafasi ya kwanza ilizawadiwa shilingi laki tano, nafasi ya pili ilishikwa na shule ya msingi  DCT Bishopstar walipatiwa shilingi laki 3 na nafasi ya tatu ilishikwa na shule ya Mlimwa C walipatiwa shilingi laki mbili huku washindi hao wakipewa ufadhili wa masomo katika shule ya ELLEN WHITE INTERNATIONAL SCHOOL iliyopo maeneo ya Nzuguni ambapo mahitaji yao yote yameghramiwa na mbunge huyo wa dodoma mjini Anthony Mavunde.
 
  NA DEVOTHA SONGORWA  DODOMA

Post a Comment

0 Comments