Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Jamii ungeni mkono utoaji huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu ili watimize ndoto zao.

WATOTO WENYE ULEMAVU WANA TIMIZIWA HAKI ZAO?:

Tumezungumza na mratibu wa kituo cha Ualimu kilichopo Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Mwl. ROBERT MASATU na BI,SARAH MWAGA yeye ni mkurugenzi wa shirika la AFNET mkoani Dodoma.

 Jamii  imetakiwa  kutoa  kipaumbele kwa wanafunzi  wenye ulemavu  ili kuondokana na dhana  potofu kuwa hawawezi kufanya vizuri katika masomo.

 Hayo yamebainishwa leo  na mratibu wa kituo cha walimu kilichopo Wilaya ya  Sengerema mkoani Mwanza (TRC)  Mwalimu  ROBERT MASATU na kusema kuwa  jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwashauri  wanafunzi  wenye ulemavu  kujiunga na masomo ya  ufundi  pale  wanaposhindwa kufaulu mitihani ya kidato cha  nne hali  itakayowajengea uwezo katika maisha yao na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Aidha  mratibu huyo ameiomba  jamii   kuwathamini watu wenye ulemavu  bila kujali aina ya ulemavu kwani  hata wao ni binadamu  kama wengine na pia wanahaki ya kuishi kama watu wengine.
Sanjari na hayo  mwalimu MASATU  amewataka wazazi  kutowaficha ndani watoto wenye  ulemavu na badala yake  wawapeleke  shule kwa manufaa yao ya badaye.
    
JE HALI HII IKOJE KWA UPANDE WA MKOA WA DODOMA?
   
Kwaupande wake  mkurugenzi wa shirika la AFNET mkoa wa Dodoma Bi,Sarah Mwaga amebainisha hali ilivyo kwa watoto wenye ulemavu mbalimbali wakiwemo watu wenye Ualbino kwa mkoa huo, kwa baadhi ya wazazi waamekuwa wakiwaficha watoto wao wenye ulemavu jambo ambalo sio zuri.

 Hata hivyo Bi, Mwaga amebainisha kwamba bado kunauhitaji mkubwa wa kuendlea kutoa elimu kwa jamii,hususani wazazi na walezi ambao wana tabia ya kuwaficha ndani wakidhani kwamba kuwa na motto mwenye ulemavu ni mkosi kwa familia jambo ambalo sikweli, kwani kila mtu anahaki ya kuishi,kusoma,kutoamaoni,kuongoza nk.

 Na.deborah.           


Post a Comment

0 Comments