Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Mbunge wa Jimbo la Mororogoro mjini Abood ameishukuru serikali kwa kutekeleza ombi lake la kutoa mashine ya X-Ray ambayo itawasaidia wananchi wakiwepo watoto.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Abdulazizi Abood, amewatembelea watoto waliolazwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, baada ya kufika ili kuona mashine ya kisasa ya kutoa huduma ya X- Ray iliyoletwa na serikali ili kuwasaidia wananchi wakiwepo watoto mkoani humo.

Ziara hiyo ya kutembelea hospitali hiyo imefanyika hivi karibuni na baada ya hapo amevitembelea vituo vya Afya katika Manispaa ya Morogoro huku ameishukuru Serikali, kwa kutekeleza ahadi yake hiyo na kuwajali wananchi wa mkoa wa Morogoro kwa kuleta mashine ya kisasa kwa ajili ya huduma za X-ray kwani kilikuwa ni kilio Cha muda mrefu ambacho amekuwa akiiomba Serikali kuwasaidia kifaa hicho.  .

Aidha Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, Dkt. Ritha Lyamuya alisema kuwa, mashine hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kazi hali ambayo imesaidia,kupunguza malalamiko ya wagonjwa ambao walikuwa wakikosa huduma ya X-ray kutokana na mashine iliypokuwepo awali kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi.
Alisema mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi na hivyo kusaidia, kupunguza idadi ya wagonjwa ambao, walikuwa wakipewa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili, kwani mashine hiyo ina uwezo wa kutuma taarifa za mgonjwa kwa njia ya mtandao na kurejesha majibu ndani ya muda mfupi.


Na Shua Ndereka, Morogoro.

Post a Comment

0 Comments