Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Mwanaume mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kumbaka mwanae wa miaka 11.

Jeshi la Polisi mkoani njombe linamshikilia mkazi mmoja  wa  mtaa  wa  JOSHONI, HEZRON  NDONE  mwenye umri wa  miaka 44 kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wake mwenye umri wa miaka 11. 

Kamishna msaidizi wa jeshi la  Polisi  mkoa  wa  Njombe,  HAMIS ISSA   amethibitisha  kukamatwa  kwa  mtuhumiwa  huyo bwana HEZRON  NDONE ambaye ni mfanyabiashara  wa  mkaa ambapo tukilo hilo limetokea mnamo January mosi  mwaka  huu.

Kamanda ISSA  amesema  taratibu  zitakapo kamilika  Bwana  NDONE  atapelekwa  mahakamani  kujibu  tuhuma  hizo  na  kuwataka  wananchi kukemea  tabia  ya  kuwaingilia  watoto kimapenzi ili kuondoa udhalilishaji katika  jamii.

Tanzania Kids Time imezungumza  na  motto mwathirika wa tukio hilo ambae jina lake limehifadhiwa amesema kitendo cha kumuingilia kimapenzi kimekuwa kikifanyika usiku wakati wadogo zake wakiwa wamelala.

Nae mama  wa mwathirika wa  tukio  hilo Bi, VALENTINA  MKORONGO  akizungumza kwa  uchungu na hisia za masikitiko  amesema  mme  wake  alimfukuza  asilale chumba  walichokuwa  wanalala  na baba  huyo kuanza kulala  na  binti yao.
Baadhi ya  majirani  wa  familia  ya mtuhumiwa HEZRON  NDONE wamesema tetezi za mtuhumiwa  kuwa  na  mahusiano na  mtoto  wake  walikuwa wanazipata  kutoka  kwa  mke wake akilalamika  na kushauri kuwa wazazi wa mme wake NDONE ndiyo wenye kumaliza tatizo  hilo.

Afisa ustawi  wa  jamii  mkoa  wa  njombe  Bi, TELESIA  YOMO amesema  vitendo  vya  ubakaji  na  ulawiti  kwa  watoto  wadogo  kuanzia  mwezi wa julai, 2019 mpaka kufikia mwezi  desemba zilikuwepo kesi 25 na  mwezi wa julai 2019 hadi january 23 mwaka huu mkoa wa njombe umekuwa na   kesi 27 za ulawiti na ubakaji. 

Jeshi la polisi kwa kushilikiana na wananchi mkoani njombe wanaendelea kutekeleza  darubini ya  dira  ya  maendeleo  ya  Taifa ya  mwaka 2025, inayosema KUWEPO KWA MAZINGIRA YA  AMANI ,USALAMA NA  UMOJA.

MICHAEL NGILANGWAPost a Comment

0 Comments