Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Mwendelezo kutoka njombe, kesi ya baba alie mbaka mwanae mwenye umri (11), baada ya kusomwa kesi yake amekana kuhusika na makosa yote manne.Ikiwa ni siku chache zimepita tangu kukamatwa kwa  mwanaume mmoja alie mbaka mtoto wake amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoani njombe na kusomewa mashtaka manne, mawili yakiwa ya kubaka na mawili yakiwa ya kumlawiti mwanae mwenye umri wa miaka 11.

Mwanaume huyo alie julikana kwa jina la EZRON NDONE mwenye umri wa miaka 44 mkazi wa mtaa wa JOSHONI kata ya MJI MWEMA mkoani Njombe, amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi HASSAN MAKUBE   na kushtakiwa kwa makosa manne mawili ya kubaka na makosa mengine mawili ya kumlawiti mtoto wake  mwenye umri wa miaka 11 .

 Aidha Akisoma shauri hilo wakili wa serikali ELIZABETH MALLYA akishirikiana na ANDREW MANDWA wamesema mtuhumiwa EZRON NDONE anashtakiwa kwa makosa manne mbapo kosa la kwanza na la pili ni kuzini na mwanae   katika siku na tarehe isiyofahamakika kinyume na kifungu cha 158 kifungu kidogo cha kwanza  (a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 ya marejeo ya mwaka 2002.

Kosa la tatu na la nne ni la ulawiti ambapo anadaiwa  kumwingilia mwanae kinyume na maumbile  kosa ambalo ni  kinyume na kifungu namba 154 kifungu kidogo cha kwanza ( a) na kifungu kidogo cha pili cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002 kikisomwa pamoja na kifungu namba 185 cha sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009.

Mtuhumiwa HEZRON NDONE amekana kuhusika na makosa yote na kurudishwa Rumande kwa kuwa mahakama imeshindwa kutoa dhamana kutokana na kuhofia usalama wa mtuhumiwa, na usalama wa ndugu  wanaohusika na mtuhumiwa.

Baadaye mawakili wa serikali wakaiambia mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuiomba mahakama kupanga siku ya kuanza kusikiliza maelezo ya awali  na hatimaye kesi ikaahirishwa   mpaka mwezi februari tarehe 5  mwaka huu.

Na Michael Ngilangwa-Njombe.

Post a Comment

0 Comments