Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ni muhimu mwanamke kujishughulisha na kilimo ili kuikomboa familia.


Wanawake wilaya ya  sengerema mkoani mwanza wameonesha  muitikio chanya katika  sekta  ya  kilimo baada ya kuona ndio sehemu ya kujipatia kipato na kusomesha watoto.

Wakizungumza na TKT Radio  wanawake wa kata ya BUSISI wamesema sekta ya kilimo  ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo na kuweza kutunza familia na kuondokana na utegemezi.

Licha ya kuwapatia kipato sekta ya kilimo lakini bado wanakutana na vikwazo mbambali ikiwemo mazao kuharibiliwa na wadudu ambao imekuwa ikiwarudisha  nyuma katika sekta hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa AMCOS, Bi MARIAMU MASHIMBA MALALE amesema wameendelea kutoa elimu kwa wakulima wa eneo hilo ili kuakikisha wakulima wanafata taratibu ambazo zinatolewa na wataalamu.

EDWIN KYARUZI ambaye ni afisa kilimo kata ya BUSISI amesema changamoto wanakutananazo wakulima ni nyingi ikiwemo kuwa na shughuli mbalimbali za kifamilia, kutoshirikishwa katika mauzo ya nafaka kutokana na baadhi ya wanaume kuwa na mfumo dume na kuwataka wajitambue zaidi.

Elimu imeendelea kutolewa na wataalamu wa kilimo katika kijiji cha BUSISI  jinsi ya kulima kilimo cha kisasa na sikulima kwa mazoea.

Deborah Maisa mwanza.Post a Comment

0 Comments