Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

TAASISI BINAFSI YA EMFERD KUTOKA MOROGORO, IMEITAKA JAMII KUWAPA KIPAUMBELE WATOTO WENYE ULEMAVU.

Taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na kulea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo Mkoani Morogoro (EMFERD), imeitaka jamii kuhakikisha inawapa kipaumbele watoto wenye mahitaji maalumu katika huduma za kijamii, ilikutengeneza  usawa na makundi mengine.

 Hayo yamebainishwa na Mlezi mshauri wa taasisi hiyo, Bi. JOSEPHINE BAKITA wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, huku akibainisha kuwepo kwaTamasha la watoto wenye ulemavu litakalofanyika Februari 7 mwaka huu, kwa kushirikiana na Kanisa Katoliki Parokia ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.

  Aidha Bi. JOSEPHINE amesema lengo la hafla hiyo ni kuikumbusha jamii sambamba na kuyakumbusha makanisa, madhehebu yote ya dini na wadau mbalimbali kuwasogeza karibu watoto wenye mahitaji maalumu na kuwapa nafasi zambelesawanawatotowengine “malengo mengine ya hafla hiyo kubwa ya Usiku wa Mwanga (Night to Shine),  ni kutoa kichocheo kwa makanisa, kuanza au kuongeza huduma ya kwawatu wenye mahitaji maalumu, kuruhusu wageni rasmi wa usiku wa Mwanga na Familia zao kuwa sehemu ya kanisa na jamii ili wahisi kupokelewa, kupendwa,  kuugwa mkono na jamii kimwili na kiroho”. Amesema Josephine.

Hata hivyo JOSEPHINE amewataka wadau mbalimbali, kuwaunga mkono,  kuwawezesha ili kufanikisha tamasha hilo pamoja na kujitokeza kwa wingi siku ya Tamasha ili kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanakuwa sawa na watu wengine.
Kwa upande wake msemaji wa taasisi hiyo VICTOR MAKINDA amesema kuwa, katika tamasha hilo,  kutakuwepo na michezo mbalimbali kwaajili ya watoto hao wenye ulemavu,  huku wakivishwa mavazi ya wafalme na malkia pamoja na kutembea kwenye zuria jekundu “kutakuwa na michezo midogo midogo kulingana na uhitaji  wao maalumu pamoja na kucheza muziki laini wenye mguso wakiimani” amesema VICTOR MKINDA.
 Tamasha la Usiku wa Mwanga (Night to Shine), lilianzishwa na mcheza Mpira maarufu wa nchini Marekani, Tim Tebow ambaye ndiye Rais wa Shirika hilo ambapo huadhimishwa kila ifikapo Februari 7 katika nchi mbali mbali Duniani, likilenga kuwapa heshima na hadhi ya juu watu wenye mahitaji maalumu hususani watoto wenye ulemavu.
Na, Shua Ndereka

Post a Comment

0 Comments