Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

kutoka wilayani mvomeroTabia ya Utelekezaji kwa wanawake na familia kutoka katika jamii za kawaida hadi kufika kwa jamii za kifugaji wa kimasai jambo ambalo lilikuwa gumu kwa jamii hiyo. Tkt/Un Radio imetembelea katika kijiji cha Mangae Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kwa asilimia kubwa eneo hilo huishi wafugaji  jamiii ya Kimasai, nakuzungumza na jamii hiyo kuhusu namna wanavyokabiriana na maisha ya kutunza familia zao hususani kuwapatia mahitaji muhimu,Ikiwemo Elimu,Afya,Lishe bora na hata michezo inayo hitaji kuchangamana na watoto wajamii zingine, na jinsigani baba wafamilia anashiriki kutunza watoto.

  Ester Obote mkazi wa kijiji cha Mangae mama mwenye watoto sita(6) amesema mmewake alifariki mwaka 2016 akamuachia watoto wawili (2) shemeji yake akachukua jukumu la kuhudumia familia ya marehemu kutokana na utaratibu wa jamii hiyo ya kimasai na wakabaatika kuzaa watoto watatu,lakini hata huyo amemtelekeza akiwa na mimba ya karibu kujifungu.

  Aidha Bi, Ester amebainisha kwamba kwasasa anahangaika kutunza watoto wake kwani mmewake wa kwanza hakumuachia urithi wowote ambao ungeweza kumsaidia kwa kipindi hiki, kazi yake kubwa anayo ifanya Kushona Shanga,na kukata miti na kuchoma mkaa iliaweze kupata pesa ya kumsaidia mahitaji ya muhimu kamavile chakula,mavazi,elimu na kuweka akiba kidogo kwa ajili ya kumsaidia wakati wakujifungua.

 Hata hivyo Mariamu Motoswa ametoa wito kwa wanaume wenye tabia ya kuwatelekeza wake zao jambo hilo linahafifisha ukuaji wakiuchumi,elimu na ustawi wa Taifa kwani tabia za aina hiyo sio tu kwa jamii za kawaida bali hata jamii za  Kimasai watu wenye tabia hizo wapo.

Post a Comment

0 Comments