Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Vilio na Simanzi vya tanda katika kijiji Cha Iyogelo Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita baada ya watoto wawili kufa kwa kusombwa na maji mnamo dec 31 mwaka jana.


                                                           

 Watoto wawili wanasadikika kufa maji baada ya kusombwa na maji ya mto wakati wakiogelea katika mto huoWilaya ya Mbogwe Mkoani Geita .
Tukio hilo limetokea mnamo Desemba 31 mwaka 2019 katika kijiji Cha Iyogelo majira ya saa sita mchana katika mto Nikonga unaotenganisha Wilaya mbili Mbogwe na Geita,watoto hao ni Idiamin Fikiri na Soba Juma wote walikuwa na umri wa miaka 15 wakazi wa kijiji cha Ikunguigazi, Tukio hilo limetokea baada ya watoto hao kumaliza kazi ya kupandikiza mpunga jirani na mto huo,

Aidha Baba mzazi wa watoto hao amesema tukio la kufa maji katika familia yake si lakwanza kwani kapoteza Mtoto na mama Mzazi katika mto huo huo Mwaka  2018, ambapo Dec 31/2019 amepoteza Mtoto mwingine jambo linalo msikitisha nakudhani kwamba hakuna .
 
 Wakizungumza na TKT RADIO baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakati watoto wenzao wakizama na walifanya jitihada za kuwaokoa  lakini ilishindikana kutokana na mto huo kujaa maji kupita kiasi,Hata hivyo Mwenyekiti wa kijiji hicho ndg Jumanne  Manyasa, Amesema matukio ya kufa maji kwa wananchi wake imekua ni kila mwaka mto huo unakatisha uhai wa wananchi Na amewaomba wananchi kuwa tahadhari pindi wanapovuka mto huo na Akasema juhudi za kupata miili ya watoto hao zinaendelea.

                   Na Nichoraus Lyankando Geita 

Post a Comment

0 Comments