Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wanawake wa Jamii ya kifugaji Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro wachangamkia bishara ya kuuza maziwa ili kuwatimizia watoto mahitaji ya shule.

Wanawake wa jamii ya Kimasai Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro wameonesha muamko wakujishughulisha na biashara ndogondogo ili kuwatimizia mahitaji muhimu watoto wao.

Hayo yanajili baada ya Tanzania Kids Time kuwatembelea baadhi ya wanawake wa kimasai katika kijiji cha WAMI SOKOINE kata ya Dakawa , MARIA SHABARA na EVA JOSHUA  amabao wanauza maziwa na kufuga kuku wamesema watoto ni hazina ya Taifa la kesho hivyo lazima watimiziwe mahitaji.

Uchumi wa familia unaanzia kwa Mama na bado wanawake wakimasai hawajachelewa  kuwatengenezea mazingira mazuri watoto wao, ili wasome na kukua wakiwa maridadi,amesema SIMON ROTI mwananchi mkazi wa Kitongoji cha KANISANI akitoa ushauri kwa wanawake.

Bwana KIFUTUTWARO KIBASISI ni mwenyekiti wa Kijiji cha WAMI SOKOINE amewapongeza wanawake wa kimasai kwa kujishughulisha ili kuwasaidia watoto na kwamba sasahivi jamii kubwa ya kimasai haina tena sababu ya kutowasomesha watoto wala kusingizia ukosefu wa mahitaji.

Wanawake hao wajamii hiyo wamewaomba wadau wakubwa wa biashara kujitokeza kuwatafuti masoko kulingana na Maziwa mengi kukosa wateja hatimaye kuharibika kutoka na kukaa muda mrefu.

Hamad Rashid


Post a Comment

0 Comments