Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Elimu ya kujikinga na Majanga ya moto imeanza kurithishwa kwa wanafunzi mkoani Tabora.
Jeshi la zima moto na uokoaji kwa kushirikiana na Dawati la jinsia pamoja na Idara ya maendeleo ya jamii katika wilaya ya KALIUA mkoani TABORA limeanza kutoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto kwa wananchi.

Kaimu kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji wilaya ya KALIUA, SAJENTI GODFREY MAGANGA amesema kupitia mikutano ya hadhara amewataka wazazi kuwa karibu na watoto kwa kuwakanya kuogelea na kucheza karibu na madimbwi akiongeza kwa kusema elimu hiyo wamekuwa wakiitoa kwa wanafunzi mashuleni. 

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii mratibu wa mfuko wa wanawake, vijana na walemavu Wilaya ya KALIUA,  ANTONY NSOLLO amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani KALIUA wameamua kutoa elimu ya malezi kwa wazazi ili kuepusha vifo vitokanavyo na watoto kudumbukia kwenye madimbwi hatimaye kufa.

Mmoja wa wananchi walioshiriki kwenye mkutano uliofanyika katika kata ya KALIUA, VAILETH LUSESA ameomba elimu hiyo iwe endelevu.  
Nao LUDOVICK KULWA na NEEMA MSANGI wamesema elimu hiyo itakuwa na tija katika jamii.

Jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya KALIUA kwa kushirikiana na dawati la jinsia pamoja na idara ya maendeleo ya jamii wilayani hapa limetoa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto katika kata za USHOKOLA, KALIUA na UFUKUTWA. 


     Na: Simon Jumanne Kaliua

Post a Comment

0 Comments