Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Kukosa Lishe bora, kupata maradhi ya mara kwa mara imeelezwa kuwa chanzo cha mtoto kudumaa akili.

Imeelezwa kuwa  chanzo kikuu cha  mtoto  kudumaa akili ni kukosa lishe bora, kupata maradhi ya mara kwa mara  na kutokuwa na makuzi mazuri.

Hayo yameelezwa katika mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa na Shirika la umoja  wa mataifa  Elimu, sayansi na utamaduni-UNESCO kwa wazazi na walezi  katika  Ukumbi wa ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya IBISABAGENI Wilayani SENGEREMA ambapo mwezeshaji  wa mafunzo  ADAM SALUM  anasema mtoto  akikosa lishe bora   hatakuwa na makuzi mazuri , uwezo wa akili  kudumaa  pamoja na kupata maradhi ya mara kwa mara.     
  
Naye Afisa maendeleo ya Jamii katika  Halmashauri ya Wilaya ya  SENGEREMA  ambaye pia ni mratibu wa mradi  huo unaofadhiliwa na UNESCO   Bwana ABELL BARNABAS amewataka  wazazi na walezi walioshiriki mafunzo hayo kwenda kuyafanyia kazi ipasavyo Elimu ya mafunzo pamoja na kuwa mabalozi wema   katika jamii.

Washiriki wa mafunzo  hayo pamoja na kuwashukuru   wawezeshaji  wa mafunzo   chini ya shirika  la  unesco wameahidi kwenda kuyafanyia kazi  walichojifunza ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto katika mazingira rafiki.

Aidha  Jumla ya  wazazi na walezi Hamsini  wamepatiwa  mafunzo ya siku mbili  juu ya makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya mtoto  katika kata ya  IBISABAGENI Wilayani Sengerema.       

Na Deborah  Maisa -Mwanza

Post a Comment

0 Comments