Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ndoa zaidi ya 50 zaomba kuvunjwa kilamwezi bukoba,huku watoto wakiwa wanga wakubwa.


Watoto wako kwenye wakati mgumu baada ya wanandoa kuachana, hayo yamebainishwa na afisa ustawi wa jamii manispaa ya Bukoba Jaffety Kanoni wakati wamahojiano maalumu na TKT na kueleza kuwa lipo ongezeko kubwa la mashauri yanayofikishwa ofisini kwake ya wanandoa au familia wanaohitaji kutengana. 

 Aidha kwa mwezi amekuwa akipokea mashauri zaidi ya 50 ya aina hiyo huku akizitaja sababu zinazopelekea kutokea kwa hali hiyo kuwa ni pamoja na hali ngumu ya kiuchumi ambapo wanaume wanapoona mzigo wa kutunza familia umekuwa mkubwa wanakimbia, huku wanawake wakitamani kuachana na waume zao na kuwatafuta wanaume wenye uwezo wa kuwahudumia wakati huo wanaoteseka zaidi ni watoto.

 Hatahivyo ameongeza kuwa sababu nyingine ni wanandoa kuamua kuingia kwenye ndoa bila kujuana kwa undani kitabia, Mabadiliko ya mfumo wa maisha unaopelekea maisha kuwa magumu na kushuka kwa nidhamu/heshima kwa wanandoa wenyewe.

Bw,Kanoni amesema kuwa matokeo yake yamekuwa mabaya kwa familia kwani yanafanya watoto kukosa malezi ya pande zote mbili na kushindwa kupata matunzo ya kutosha hasa kwa zile familia ambazo wanaume anakuwa amekibia.

Bi,Dativa Edward ni mkazi wa mtaa wa Buyekera Manispaa ya Bukoba yeye amekimbiwa na mume wake miaka miwili iliyopita na kumuachia watoto wawili anasema kuwa anapata ugumu wa kuwalea watoto hao kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuwahudumia.

Hatahivyo licha ya kumpeleka mume wake kwenye vyombo vya sheria na kuamuriwa achangie kiasi cha shilingi elfu 5 kila wiki kwa ajili ya watoto alikataa kutekeleza maelekezo hayo nakuamua kuhama mji alipokuwa akiishi.

Wakili kutoka shirika la msaada wa kisheria la MUHOLA mkoani Kagera Bi,Telesia Bujiku anakiri pia shirika hilo linayo malalamiko mengi ya wanaume kukimbia familia zao ambapo anashauri wanandoa wengi watumie njia ya uzazi wa mpango ambayo itawasaidia kuwa na watoto wanaoendana na kipato chao.

Pia amewashauri wanawake kujenga tabia ya kufanya kazi na kuondokana na utegemezi wa kila kitu kwa waume zao, na kwamba iwapo wanaume na wanawake watashirikiana katika kutekeleza majukuu ya kifamilia itasaidia kudumiasha maelewano.

Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba waliozungumza na kids Times wamesema kuwa jamii bado inahitaji elimu ya malezi na makuzi ya watoto itakayoonyesha athari za watoto kulelewa na mzazi mmoja na kwamba kuongezeka kwa wanandoa kutengana kunatokana na kupuuzwa kwa mila na desturi na kukubali mifuo ya kigeni

Na,Rosemary Elias-Kagera.

Post a Comment

0 Comments