Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

SERIKALI IMETAKIWA KUIMALISHA ULINZI KWA WATOTO WENYE UALBINO NJOMBE


Serikali Mkoani Njombe imeshauriwa kuimarisha ulinzi katika shule na vituo vya kulea watoto wenye Ualbino, kwa kuwajengea Uzio utakaosaidia ulinzi, usalama, kuwakinga na maadui.
Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wachungaji Kutoka kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) mkoani Njombe akiwemo Melinze Tweve, baada ya kuzungumza na TKT/UN Radio kuhusiana nna usalama wa watoto hao katika kuelekea kipindi cha Uchaguzi mkuu 20202, ambaye amesema uzio unapojengwa au kuzungushwa katika shule utasaidia ulinzi juu ya watoto wenye Ualbino.
“watu wanaamini imani potofu ndiyo maana wanafanya mauaji ya watu wenye Ualbino, mambo ya mila wanadanganywa na waganga wa kienyeji kwamba utajiri unapatikana kwa njia hiyo lakini utajiri unapatikana kwa kumtegemea Mungu” amesema
Mchungaji Gervas Chanyama wa kanisa hilo pia amesema kujenga uzio itasaidia kuzuia watu wabaya ambao bado wanaimani potofu juu ya watu wenye Ualbino, hivyo serikali iendelee kuweka ulinzi juu ya watoto na watu wote.
“kuwepo na uelimishwaji wa jamii yetu ili wajue watoto hawa wanahitaji kulindwa, kuheshimiwa na kupata malezi bora hivyo kujengwa kwa Uzio kutasababisha kuwepo lango kuu ambalo litakuwa na ulinzi ambao utasaidia kuepusha wahalifu kuwafikia” 
Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto wenye Ualbino Bi. Beth Liduke amesema serikali na wadau wanapaswa kutambua umuhimu wa kuzungushia uzio kwenye shule na vituo vinavyolea watoto hao ili kuimalisha ulinzi na usalama.
“kwa watoto ambao wanaualbino na uono hafifu ambao wapo kwenye shule maalumu wanahitaji ulinzi wenye uhakikia, kama zipo shule zenye watoto hao na hazina uzio usalama wao ni mdogo..lakini nishauri viongozi wa shule hizo wahakikishe wana uzio kwa ajili ya usalama wa watoto” amesema.
Kwa upande wake, Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Njombe Averino Chaula amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwajengea Uzio kwenye shule zenye watoto wenye Ualbino pamoja na vituo vinavyowalea.
Hata hivyo Mbunge wa jimbo la Lupembe Joramu Hongoli ameshauri wadau na serikali kutengeneza mazingira rafiki ya shule za watoto wenye Ualbino ili kuimarisha ulinzi dhidi ya kundi hilo, pamoja na wananchi kukemea matendo hatarishi kwa watoto hao.
“shule ambazo watoto wetu wanasoma inapaswa kuwa na uzio maana watu wana roho tofauti tofauti hivyo nitoe rai kwa jamii, tusiingalie serikali tu hata wadau, wazazi na wenye mapenzi mema wanaweza kujitoa na kuchangia ili kujenga uzio kwa usalama wa watoto wote” amesema.
Na; Michael Ngilangwa- Njombe


Post a Comment

0 Comments