Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

SERIKALI ITENGE FUNGU LA KUTOSHA KUHUDUMIA WATOTO WENYE UALBINO SHULENI. Takribani Million kuminanne lakinane na ishirini Elfu zimetumika mkoani Morogoro katikaununuzi wa mafutayakupaka kwa watoto wenye ualbino.
Hayoyamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha watuwenye Ualbino mkoa wa Morogoro (TAS) HASSAN MIKAZI kwa mahojiano maalum na TKT/UN RADIO ilikujua wilaya ya Kilosa imesaidiwaje katika fedhahizo.
  
Aidha MIKAZI alisema TAS imekuwaikisaidia watoto wenye Ualbino ikiwamwa kawa 2019, wilaya ya Kilosa ilitumia kiasicha shilingi Lakisita kwa kununua vifaa kwa watuwenye Ualbino, hukushuleyamsingi Mazinyungu iliyopo Wilayani humo ikifaidika nafedhahizo.

TKT/UN RADIO iliamua kufikampaka katika shule ya Msingi Mazinyungu iliyopo Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na kukutana na uongozi wa shule hiyo pamoja na  wanafunzi wenye Ualbino ilikubaini mahitaji yao miongoni kati yahayo ni, Miwani yakujikinga na jua,Vikuzia mandishi ubaoni,Mafuta na Vitumbalimbali.

 AZIZI MSAFIRI nimwanafunzi mwenye Ualbino katika shulehiyo amesema kuwa serikali huwasaidia maramojamoja, hivyo amewaomba wadau kuendelea kuwasaidia kwani wanahitaji vifaa vingi kulingana nahali waliyonayo.

“Sisitunamavaziyetubinafsikwakipindi cha juakamakuvaamashatiyamikonomirefu, Surualindefunakofiakwaajiliyakujikinganajuahuwatunanunuawenyewetu” Alisema Azizi Msafiri.

Kwaupande wake, Mwalimu Mkuu wa Kitengo cha Elimu Maalum katika shule ya Msingi Mazinyungu ALLY NKURU amesema, licha ya kuwepo kwa changamoto kwa wanafunzi wenye Ualbino, wengiwao wana uwezomzuridarasani kwaniwanaomaliza Elimu ya msingi wanafanikiwa kujiunga nasekondari.

“mbali nahilo zipochangamoto zingine kama vile  kuchelewa kwavitabu, walimu wachache pamoja naidadi yawanafunzi kuwa kubwa hivyo inawawia vigumuwaalimu katika ufundishaji”alisemaAlly Nkuru

ASAJILE MWAMBAMALE ambayeni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Kilosa ameelezea mikakati yao katika kushughulikia suala la mahitaji yawanafunzi wenye Ualbino kwenye halmashauri hiyo kwamba Bajeti ya Serikali kutoka Ofisi ya Rais tawala zamikoa na Serikali zamitaa TAMISEMI wanatenga fungu kwaajili ya wanafunzi hao wenye mahitajimaalumu.

“tunapataluzuku mojakwamoja tumekua tukipata takribani zaidi ya Milioni miamoja na ishilini kwa ajili yawanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo watoto wenye Ualbino”Amesema ASAJILE MWAMBAMALE.

 Pia Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo Hamidu Ally amesema Bajeti ya Serikali haikidhi mahitaji ya wanafunzi wenyemahitaji maalumu, kwasiku hadi siku inaendelea kupunguzwa, hivyo wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kwaajili ya kulisaidia kundi hilo la watoto wenye mahitaji maalumu ilikuwasaidia kutimiza ndoto walizo nazo.

 Hatahivyo Mwenyekiti wa Chama cha watuwenye Ualbino mkoa wa Morogoro (TAS), HASSAN  MIKAZI amewaomba wadau mbalimbali,Mashirika binafsi,Watu watakao guswa wajitokeze kuchangia  watoto wenye Ualbino waliopo shuleni ilikupata vifaa vinavyo hitajika kwa kilasiku, kwani fungu la pesa linalo tengwa kwa Mkoa wa Morogoro bado halikidhi mahitaji kwa watu wenye Ualbino.

Na: John Kabamabala-Kilosa Morogoro.

Post a Comment

0 Comments