Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Shule ya msingi IGOGO wilaya ya Sengerema imeandikisha watoto wa Darasa la awali 288.


Shule ya msingi IGOGO imevuka  lengo la uandikishaji wa watoto wa Darasa la awali kwa kuandikisha wanafunzi 288 badala ya 215.

Hayo yamebainishwa na mwalimu  mkuu msaidizi wa shule IGOGO Bi,ESTHER JOSHUA ambapo amesema idadi kubwa ya watoto wa awali imeongezeka huku akidai kuwa lengo lao limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia therathini.

Hata hivyo Bi JOSHUA amesema  ili kuahakikisha idadi ya watoto inaongezeka lazima washirikiane viongozi wa Serikali za mitaa  kwa ajili ya kutambua idadi ya watoto wenye umri wa miaka minne hadi miaka mitano hao ambao bado hawajaandikishwa darasa la awali. 

Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wa awali   Bi JOSHUA amewaomba wadau mbalimbali wa elimu kufika katika shule hiyo na kutoa michango kwani bado inakabiliwa na upungufu wa miundo mbimu. 

Aiha zoezi hilo bado linaendelea la uandikishwaji wa watoto wa awali mpaka march 30 mwaka huu.


Na Deborah                                           
                                  


Post a Comment

0 Comments