Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Ujenzi wa vyoo katika baadhi ya shule kwenye halmashauli ya BUKOBA vijijini bado ni changamoto.

Baadhi ya shule katika halmashauri ya wilaya ya bukoba vijijini mkoani kagera bado ni changamoto kubwa hayo yamebainishwa katika baraza la madiwani wa halmashauri hiyo .
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwa afisa mipango wa halmashauli hiyo  Bwana JULIAN TALIMO wakati akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2020\2021 ambapo amesema katika mwaka huu wa fedha changamoto hii ya uhaba wa vyoo itatatuliwa kulingana na fedha inayotarajiwa kurasimishwa katika halmashauri.

TALIMO  ameeleza zaidi ya bilioni 56 na zaidi inategemewa kurasimishwa huku bilioni 5.8 inatarajiwa kuelekezwa katika miradi vipolo na ujenzi ikiwemo ujenzi wa matundu ya choo katika shule ili kuwanusuru watoto katika changamoto hiyo.

Hata hivyo amesema halmashauri BUKOBA vijijini ilitegemea kuandikisha watoto wa elimu ya awali jumla ya wanafunzi 11,933 huku asilimia 79% ya watoto walioandikishwa wamekumbwa na uhaba wa vyoo mashuleni.

Nae afisa elimu sekondai  Halimashauri hiyo Bwana, CHACHA MEGEWA ameongeza kua licha ya kuwepo kwa changamoto ya vyoo mashuleni  lakini pia kuna changamoto ya wanafunzi kupata mimba kabla ya kumaliza elimu yao.

CHACHA amesema wanafunzi waliotambuliwa kupata mimba kwa upande wa sekondali wapo 18 kwa mwaka uliopita huku kwa mwaka huu sasa inakadiliwa  zaidi ya wanafunzi 10 tayali wamebeba mimba katika shule mbalimbalindani ya halmashauri hiyo. 
Na Silvia Amandius.


Post a Comment

0 Comments