Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Visiwa vitano Mkoani KAGERA vimepunguza Vifo vya akina mama na watoto.
Takribani visiwa vitano Mkoani KAGERA vimepunguza vifo vya akina mama na watoto pamoja na changamoto za miundombinu zilizopo.

Mganga mkuu wa Mkoa wa KAGERA, HASSAN MOHAMMED alisema Idadi ya vifo upande wa visiwani kwa akina Mama mwaka 2018 vilikuwa 65 na mwaka 2019 vilikuwa 53  lakini pia kwa upande wa Watoto mwaka 2018 vilikowa 70 na mwaka 2019 vilikuwa 65.

HASSAN MOHAMMED alisema Idadi ya wanawake na watoto walioko katika visiwa hivyo ni inakadiriwa milioni tatu wakati vituo vya afya vilivyopo bado havikidhi kuhudumia idadi ya wakazi waliopo sambamba na kuwepo kwa watumishi wachache wa Afya katika vituo vilivyopo.

Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Afya  maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto Daktari ZAINABU CHAURA akiwa ziara ya kikazi mkoani Kagera alisema Serikali inafanya jitihada kuhakikisha inaokoa vifo vya akina mama na watoto na kuweza kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi wa afya na vituo vya Afya.

Amewashukuru watumishi wa Afya aliokutana nao na kuwataka kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa bidii kutokana na kazi hiyo kuwa kazi ya wito pia kuwataka waendelee kukabiliana na changamoto wakati Serikali ikizishughulikia.

Kwa mujibu wa mganga mkuu wa Mkoa wa KAGERA HASSAN MOHAMMED Takwimu zinzonesha kati ya visiwa  32 vilivyopo ni visiwa 26 wanavyoishi watu ambapo visiwa vitano vya GOZIBA, BUMBILE MAZINGA, IKUZA na KEREBE, vinaongoza kuwa na idadi kubwa ya vifo vya akinamama na watoto.


Na Silivia Amandius -Kagera
 


Post a Comment

0 Comments