Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Vituo vya Radio vimetakiwa kuboresha maudhui mazuri ya vipindi vya watoto.
Vituo vya Radio nchini vimetakiwa kuwajibika kikamilifu kutoa vipindi vinavyohamasisha  makuzi na malezi bora ya mototo. 

Hayo yamezungumzwa na  MARIA NGOMBALE pamoja na SEMBONANGA JUMA ambao ni wazazi na walezi kutoka Manispaa ya Morogoro ambapo wamesema vituo vingi vya Radio kwa sasa vimekua havitoi nafasi kubwa ya vipindi vyenye maudhui mazuri kwa watoto tofauti na miaka ya nyuma.

MARIA NGOMBALE amevisihi vituo vya Radio kuweka mkazo vipindi vya watoto vyenye maudhui ya msingi na kwa wakati badala ya kucheza nyimbo zenye maadili mabaya kwa watoto.

Tanzania Kids Time imezungumza na baadhi ya watoto wanaoishi Morogoro OSCAR MATAIMBA na JOEL PHILIPO, wamesema katika vipindi vya watoto Redioni wamekua wanasikiliza muziki kwa wingi hivyo wanashindwa kupata  wanachostahili kutoka kwenye vipindi vya Radio vyenye maudhui yanayowalenga na kuwasihi waendeshaji wa vipindi vya watoto kuboresha maudhui ya vipindi vyao.

RAMADHANI CHIGALU ni mwandishi wa Habari na mtangazji kutoka Morogoro anakili vipindi vya watoto kutopewa nafasi kubwa katika mzunguko wa vipindi vya Radio lakini vilivyopo vinafanyika kwa uhakika na watanagazaji wanatimiza jukumu lao pamoja na uwepo wa teknolojia ya sasa ambayo ndio imebadili mfumo wa uendeshaji vipindi vya Radio.

CHIGALU amewataka wazazi na walezi kuendelea kusikiliza vipindi vya Radio vya watoto ili kufanyia kazi maudhui yanayotolewa.

Mwaka huu wa 2020 kaulimbiu ya siku ya Radio inasema,TUNASHEREHEKEA NGUVU YA RADIO KUTAFAKARI NA KUKUZA UTOFAUTI WA AINA ZAKE ZOTE.

Pia ujumbe kutoka kwa mkurugenzi wa shirika la Umoja wa mataifa la Elimu,sayansi na utamaduni UNESCO. Bwana AUDREY AZOULAY katika kuadhimisha siku hii ya Radio unasema, mbinu tofauti za kusambaza taarifa kupitia redio iwe ni katika mita bendi ya AM au FM au kwa kupitia teknolojia za kidijitali au kwenye wavuti zinaendana na utofauti katika yaliyomo kwenye programu ambazo zinazalishwa na wingi wa maoni, utamaduni na yale yanayotangazwa.Na Hamad Rashid-Morogoro
Post a Comment

0 Comments