Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wanafunzi 1,670 Wilayani KALIUA bado hawajaripoti kuanza masomo ya Sekondari.
Jumla ya wanafunzi 1,670 sawa na asilimia 34 ya waliopangwa kuripoti kuanza masomo ya sekondari january 2020 katika wilaya ya KALIUA mkoani TABORA bado hawajaripoti huku Serikali ikiahidi kuchukua hatua dhidi yao.

Akizungumza na TKT Radio Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya KALIUA, Daktari JOHN PIMA aliesema wanafunzi 4,879 wamefaulu kuanza masomo ya sekondari ambapo mpaka sasa wanafunzi 3,209 sawa na asilimia 66 ndio pekee walioripoti shule. 

Alisema wazazi ambao bado hawajakamilisha mahitaji ya watoto wafike kuuona na uongozi wa shule ili kuepuka kuchukuliwa hatua.

Afisa Tarafa ya KASHISHI, DANIEL SALAMBA alisema kufunguliwa kwa shule mbili za sekondari kwenye Tarafa yake imekuwa chachu kwa wazazi kuwapeleka shule watoto.

SALAMBA alizitaja Shule zilizopokea anafunzi mpaka sasa ni ELEGE Sekondari wanafunzi 69 kati ya 84, SELELI wanafunzi 86 kati ya 113 huku shule kongwe ya KASHISHI wanafunzi walioripoti ni 211 kati ya wanafunzi 260.

Nao Afisa Tarafa ya KALIUA, BETHOD MAHENGE pamoja na Afisa Tarafa ya MWONGOZO, JACKSON ZACHARIA walisema ni vyema wazazi wakaunga mkono mpango wa elimu bure kwa kuwapeleka watoto shule.

Miongoni mwa shule ambazo uripoti wa wanafunzi ni hafifu ni pamoja na ZUGIMLOLE SEKONDARI ikiwa na asilimia 55 ya wanafunzi ambao bado hawajaripoti, IGWISI sekondari asilimia 51, na ULYANKULU sekondari asilimia 47.

Na:Simon Jumanne -TABORA

Post a Comment

0 Comments