Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wananchi Mkoa wa TABORA waanza mchango kujenga vyumba vya Madarasa kunusuru wanafunzi wasikae chini.

Wananchi katika kata ya KAZAROHO wilaya ya KALIUA mkoani TABORA wameazimia kutoa mchango wa shilingi elfu mbili mia tano kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari KAZAROHO.

Awali akisoma taarifa ya miradi iliyopo katani humo Afisa mtendaji wa kata ya KAZAROHO, OMARY MASAKA amesema upungufu wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari KAZAROHO ndiyo sababu ya kuwataka wananchi kutoa mchango wa shilingi 2500 kwa ajili ya ujenzi.

Amesema kutokana na gharama za mchango kuwa kiasi kidogo ametoa mwito kwa wananchi kuwa wepesi wa kutoa mchango huo.
WILIAMU SIMON ni mkazi wa kijiji cha KAZAROHO amesema kutokana na shule ya sekondari kupokea wanafunzi kutoka kata jirani ya USIMBA ameomba pia wananchi wa kata hiyo kushiriki kwenye mchango huo huku afisa mtendaji wa kata akisema mchango huo utahusisha wananchi wa kata mbili za KAZAROHO na USIMBA.

THERESIA SOTERI ni mkuu wa shule ya sekondari KAZAROHO amesema wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ni 187 huku akibainisha uhitaji wa madarasa.
Kwa mjibu wa makubaliano ya wananchi mwisho wa kutoa mchango huo ni March 30 mwaka huu. 

Na:Simon Jumanne - Tabora

Post a Comment

0 Comments