Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Watoto 224,364 sawa na asilimia 39.8 mkoani Kagera wanakabiliwa na utapiamlo, Ikiwa imeshuka kutoka asilimia 41.7 kwa mwaka 2018/19. Afisa lishe mkoani Kagera Bw,Yusuf Hamis ameiambia Tanzania Kids Time kuwa moja ya sababu kubwa inayoelekea mkoa huo kukabiliwa na utapiamulo ni kutokana na kutokutolewa kwa  fedha zinazotengwa na halmashauri kwa ajili ya afua za lishe, kama miongozo ya wizara inavyoelekeza kwa kila mtoto mwenye chini ya umri wa miaka 5 kutengewa fungu kwa ajili lishe.

 Aidha baadhi ya maafisa lishe Zena,Robson na Norah Nyakunga  wa halmashauri za mkoa wa Kagera wamedai kuwa kutokutolewa kikamilifu kwa fedha hizo kunasababisha shughuli zilizopagwa kwa ajili ya lishe zisifanyika kwa wakati,kwani hakuna kazi ambayo inaweza kufanyika  hivyo  nakushindwa kufikia malengo .

 Hatahivyo katibu tawala mkoa wa Kagera ambaye pia  ni wenyekiti wa kamati ya lishe Prof.Faustine Kamuzola amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuweka kipaumbele suala la lishe kama yalivyo masuala mengine na kuagiza fedha zinazotengwa kutolewa kwani udumavu wa Watoto utaathiri kizazi hiki na najambo hili linauchafua mkoa wa Kagera.

 Wadau mbalimbali wanaopambana kutokomeza utapiamlo mkoani humo moja wapo ni Dr,Magrety Ishengoma mtaalam wa mabadiliko ya lishe kutoka shirika la IMA World Health yeye amesema kwa mwaka huu wa 2020 fedha ambayo imekwisha tolewa ni milioni miasita.
 
 Udumavu unatajwa kumuathiri mtoto kimwili na kiakili ambapo uwezo wake wa kufikiri na kuchanganua mambo hasa awapo darasani unakuwa mdogo ukilinganisha na yule asiye na utapiamlo,ili kutokuruhusu hali hiyo kumkabili mtoto, ni lazima lishe izingatiwe ndani ya siku elfu 1 tangu kutungwa kwa mimba hadi miaka 2.

Na. Rosemary Bundala-Kagera.

Post a Comment

0 Comments