Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Watoto 6,690 wanakadiriwa kuwa na Virus vya UKIMWI Kagera.
Mratibu wa kudhibiti UKIWI mkoani Kagera ambaye ni Daktari wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Bukoba, Jonasy Kessy amesema watoto 6,690 wanakadiriwa kuwa na maabukizi ya Virus vya UKIMWI, ambao waliofikiwa ni 3,627 sawa na asiliima 57%,Amaeongeza kuwa watoto wanaotumia dawa za kufubaza virusi vya UKIWI ni 3,617 sawa na asiliima 97% ya waliogundulika kuwa na VVU na waliofubaza virusi vya ukimwi ni 2,769 sawa na asiliima 76%

 Aidha Dr.Kessy amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na idara hiyo umebaini kuwa asilimia kubwa ya watoto hao wamepata maabukizi kutoka kwa mama kwani baadhi yao hawafiki kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupata ushauri kabla ya kubeba mimba, na wengine walibeba mimba bila ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya jambo ambalo litahatarisha maisha yao zaidi,
“Mwanamke mwenye virus vya UKIMWI kama hatumii dawa vizuri na hafuati maelekezo ya wataalam ikiwemo kuwahi Kliniki kupimwa wingi wa Virus na Kutumia dawa kwa usahihi wanaiweka kwenye hatari ya kupata VVU mimba”alisema.

 Hata hivyo Masudi Rashidi kutoka katika manispaa ya Bukoba amewashauri wanawake walio na maambukizi ya vvu wanapaswa kuzingatia mafundisho ya wataalamu wa afya hasa kabla na baada ya kujifungu ili watoto wao wasipate maambukizi,kwani maambukizi mengi yanatoka kwa mama na mtoto.

  Baadhi ya wanawake katika  manispaa hiyo wameishauri serikali kwa sharti la kutotajwa majina yao wamesema kuna haja ya wanawake na vijana wa kike kufundishwa kuhusu elimu ya maambukizi,kwani walio wengi hawana ufahamu wa kujikinga na mimba na kuwakinga watoto wao walioko tuboni kuhusu vvu,na ilikufisha elimu hiyo kwa urahisi kwenye jamii vitumike vyombo vya habari yani Redio za kijamii,majarida maalumu,magazeti na ziandaliwe semina ngazi ya mitaa,mikutano ya vijiji pamoja na kusabaza vipeperushi vyenye ujumbe wa masuala ya uzazi kwa mama mwenye VVU ili kuepusha maambukizi mapya.

Dr.Kessy amesema kuwa bado upo unyanyapaa mkubwa kwa watoto wenye VVU ngazi ya familia na jamii unaosababishwa na wanafamilia kwa kuwaficha na kushindwa kutumia dawa kwa usahihi na kuanza kushabuliwa na magonjwa mengine yanayohatarisha afya zao na kushindwa kumudu kushiriki haki zao ikiwemo haki ya kielimu.
   Na.Rosmary Eliasi-Kagera.


Post a Comment

0 Comments