Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Watoto milioni 1.1 waliugua kifua kikuu kati yahao watoto 205,000 walifariki dunia mwaka 2018. Wastani wa watu milioni 10 waliugua ugonjwa wa kifua kikuu (TB) ulimwenguni kwa mjibu wa shirika la Afya duniani WHO . Wanaume milioni 5.7, wanawake milioni 3.2 na watoto milioni 1.1, na jumla ya watu milioni 1.5 walikufa kutokana na ugonjwa huo mnamo mwaka 2018 (pamoja na watu 251,000 wenye VVU), Ulimwenguni pote taarifa hiyo imebainisha kwamba, Kifua kikuu ni moja ya sababu 10 za vifo na sababu inayoongoza kuambukiza  kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwamwingine (juu ya VVU / UKIMWI).

Aidha Watoto milioni 1.1 waliougua ugonjwa wa Kifua Kikuu ulimwenguni, kati yahao watoto 205,000 walifariki dunia kwa sababu ya TB (pamoja na watoto walio na VVU). Kifua kikuu cha watoto na vijana mara nyingi hupuuzwa na watoa huduma za afya na inaweza kuwa ngumu kugundua na kutibu.

   Hatahivyo kwa mwaka 2018 who ilibainisha kuwa nchi 30 zenye idadi  kubwa kuwa na wagonjwa wa Kifua Kikuu zilikuwa na asilimia 87 yamaambukizi mapya ya kifua kikuu. Nchi nane zinachukua theluthi mbili kati ya hizo ni India inayoongoza kwahesabu, ikifuatiwa na, Uchina, Indonesia, Ufilipino, Pakistan, Nigeria, Bangladesh na Afrika Kusini.

Mkakati wa Kifua Kikuu who nikuhakikisha inapunguza maambukizi mapya yakifua kikuu kwa watoto na watu wazima kwa 4-5% ya kila mwaka kufikia mwishoni2020.
   Kukomesha janga la TB ifikapo 2030 ni kati ya malengo ya kiafya ya Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs. kutibu watu milioni 40 kwa ugonjwa wa Kifua kikuu katika kipindi cha miaka 5 20182022

 Who iliweka wazi badgeti yao kuwa  zinahitajika  dola bilioni 13 za Marekani kila mwaka ilikusaidia kufanya utafiti ilikubaini wagonjwa wapya wa kifua kikuu, matibabu na utunzaji ifikapo 2022.

Post a Comment

0 Comments