Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

WATOTO WENYE UALBINO WAHOFIA USALAMA WAO KILOSA.


 Kadri siku zinavyozidi kwenda hofu inazidikuongezeka kwa wanafunzi wenye Ualbino katika shule ya msingi Mazinyungu iliopo Wilaya ya Kilosa mkoni Morogoro.


Shule  hiyo yenye wanafunzi 17 wenye Ualbino wameeleza kuhofia usalama wao baada ya kutembelewa na TKT/UN Radio.

Mmoja wawanafunzi hao ni Azizi Sauka darasa la 5 amesema  usalama kwao ni muhimu kwani awali kumekuwepo natuhuma za kuuwawa kwao, hivyo wanamashaka hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu. 

“moja ya haki tunayotakiwa kupatiwa sisi watu wenye Ualbino ni kuwekewa uzio shuleni, maana anaweza kuja mhalifu akatubeba na hakuna mtu wa kujua” alisema

Maria Kigodi ni mwanafunzi wa darasa la 5 amesema wapo watu mbalimbali walifika shuleni hapo mwaka 2018/2019 kuhitaji kujenga uzio, lakini hadi sasa mwaka 2020 bado uzio haujajengwa,hivyo nakuomba wadau kujitokeza ilikujenga uzio huo.

Mkataba wa haki za watoto  uliopitishwa mnamo Novevemba 20,1989 (CRC) katika kifungu cha 23;1kinaeleza kuwa;  watoto wenye aina yeyote ya ulemavu wapewe huduma na uangalizi maalumu, ili waweze kuendeleza vipawa vyao kikamilifu na maisha ya kujitegemea, huku kifungu cha 35 kikieleza kuwa; Serikali inapaswa kuhakikisha watoto hawatekwi wala kuuzwa.

Sheria ya mtoto inatoa wajibu kwa serikali,Wazazi,Walezi na jamii kwa ujumla kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili na ubaguzi, licha ya watoto wangine wameendelea kuwa waathirika wa aina mbalimbali za ukatili, hasa ukatili wa kingono,mauwaji na ubakaji.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mazinyungu Happy Isdori amesema kuwa jambo la kukosekana kwa wigo linawapa wasiwasi huku akiwaomba wadau kujitolea ili kuwasaidia kujenga uzio katika shule hiyo.

“hicho ni kilio chetu daima kujengewa uzio, kwa jinsi ilivyo kuwaweka watoto wenye Ualbino katika hali ya usalama ni njema zadi huwezi kujua dunia ilivyo” amesema

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Mzinyungu, Hamidu Ally amesema serikali imepunguza bajeti kwa watoto wenye ulemavu wakiwemo wenye Ualbino jambo ambalo linawakatisha tamaa hasa wasimamizi wa watoto hao, kwani idadi ya wenye Ualbino kuja kusoma katika shule hiyo inaongezeka siku hadi siku.

“bajeti yake tuliandika tukapeleka halmashauri, serikali ikasema haina hizo fedha, tunahitaji sauti iwafikie Wabunge wanaoshughulika na masuala ya kutetea haki za watu wenye Ualbino, waweze kujadili”  amesema.

 Asajile  Mwambambale ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro amesema wataanza kuweka benki ya matofali yatakayo tumika kujengea uzio huo kwa mwaka ujao wa fedha 2020/2021.
“ni kweli tumekuwa na changamoto ya bajeti kama halmashauri tumejipanga kwa mwaka ujao wa fedha na kuwa na benki ya matofali kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa uzio huo”amesema.

Hata hivyo Kutokana na takwimu za ofisi ya ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro, kwa upande wa Wilaya ya Kilosa, imeeleza kuwa; watu wenye ualbino jumla ni 67 ikiwa watoto wa Kike ni (23) na Watoto wa Kiume ni (44)  huku jumla ya mkoa ni watu 132, wakike ni (60) na Wakiume ni (72) .

Na; John Kabambala-Morogoro.

Post a Comment

0 Comments