Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Wilaya ya Njombe imebainika kuwa nachangamoto nyingi za uangalizi wa watoto.


Mkuu  Wa  Wilaya  Ya  Njombe   Bi.Luth  Msafiri  amewaomba  wadau wa  Elimu  kuendelea  kujenga  vituo  vya  kulelea  watoto  Ili Kuimarisha  ulinzi , usalama na  Lishe kwa  watoto  walio chini  ya umri wa  miaka  minne.

Bi. Msafiri  Amesema  Wilaya  ya  Njombe  Inachangamoto  nyingi   za  uangalizi  watoto , akina  mama  kutumia  muda  mwingi  katika  kazi  za  biashara  na  mashambani  huku  wengine  wakikosa  wasichana wa kusimamia  utoaji  lishe nyumbani.

Aidha  amesema  katika  swala  la  Elimu  Rasmi ambapo  Maafisa  Elimu  wameagizwa  kwenda  kusimamia  na  kuchunguza  elimu  wanayopewa  watoto  waliopo  katika  vituo  hivyo  vya  Chekechea  na  vile  vinavyolea  watoto  wenye chini ya  miaka  minne.

  Bi. Msafiri  amebainisha kwamba  serikali  imegundua  kuwepo  kwa  changamoto  ya  watoto  wa  shule  za  sekondari    kusafiri  umbari mrefu  na  kusababisha  elimu  kushindwa  kutolewa  kikamilifu  kwao  kutokana  na watoto  kuchoka  kwa  safarindefu, kwani  huchelewa kufika shuleni  na hivyo  utatuzi  wake  ni kujenga  mabweni  ili  waishi kwenye maeneo ya  shule zao.

Awali akitoa  hotuba  katika  kikao cha  robo ya  pili ya  baraza  la madiwani  la halmashauri  hiyo  Makamu  mwenyekiti   Vasco  Mgunda  amesema  wanaendelea  kuboresha  miundombinu ya vyoo, madarasa na  mabweni huku akiagiza  kusimamia  wazazi kupeleka  watoto   kujiunga  na masomo ya sekondari  kwa waliochaguliwa.

Akizungumza na TKT  afisa  ustawi  wa Jamii halmashauri  ya  Wilaya  ya  Njombe  Averino  Chaula  amesema bado  wanaendelea  kuimarisha  ulinzi  na usalama  kwa  watoto  kwa  kutengeneza  mifumo  inayotoa  elimu  na ufuatiliaji  wa  matukio  ya  watoto.

Na,Michael Ngilangwa-Njombe.

Post a Comment

0 Comments