Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

WIZARA YA AFYA IMEBARIKI MSAFARA WA KUTOKOMEZA UKATILI NCHINI.


 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imebariki kuanza kwa Msafara wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Akizungumza na wawakilishi wa Wizara, Wadau kutoka Legal Services Facility, Wildaf na wasanii wa muziki wa kizazi kipya jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Leonard Mchau amesema msafara huo umeandaliwa maalum kupeleka ujumbe wa kupambana na ukatili wa kijinsia kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani.

Bw. Mchau amewaasa wawakilishi hao wa Msafara huo kupeleka ujumbe huo ambao utasaidia kuendeleza mapambano ya kutokomeza vitendo vya ukatili nchini ambavyo vimekuwa vikishamiri kila siku katika jamii.

Ameongeza kuwa Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa  kijinsia vinatokomea kwa kasi ili watoto na wanawake wanaoathirika na vitendo hivyo kuoondokana na vitendo hivyo vinavyowanyima baadhi ya haki zao msingi.

Akizungumza kwa naiaba ya Wadau Mwakilishi wa Shirika la LSF Bw. Joseph Magazi ameishukuru Serikali kwa kuwashirikisha wadau katika kampeni ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano hayo.

Msafara huu tayari umeanzia katika mkoa wa Katavi wilaya ya Mpanda tarehe 24/02/2020 na kuendelea hadi tarehe 05/03/2020 ambapo utahitimishwa mkoani Simiyu.

Na; Shua Ndereka-Morogoro

Post a Comment

0 Comments