Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Elimu kuhusu haki sawa kwa wote bado inahitajika kwa jamii.Usemi wa haki sawa kwa wote  baadhi ya maeneo na jamii nchini bado nichangamoto,ambapo mashirika,Wadau na serikali wanatakiwa  kutoludi nyuma ili usemi huu unaokuwa ukizungumzwa upatikane na kila mmoja aweze kufurahi matunda ya taifa lake.

 Elizabeth Julius ni mzazi wa watoto watatu (3) wakiume wa wili(2) na wakike mmoja (1) ambae ndio Neema mlemavu wa macho yaani (kipofu), mtoto huyu alizaliwa mwaka 2010 kwa sasa anazaidi ya miaka tisa na anasoma shule ya msingi Mazinyungu iliopo Wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro.

 Bi,Elizabeth ameeleza changamoto kubwa nikatika malezi ya mtoto huyo anapo hitaji kwenda sehemu yeyote kucheza na wenzake na ukosefu wa fimbo ya kumsaidia  kumuongoza, hivyo akaiomba jamii na taasisi mbalimbali kuendelea kuwasadia watoto wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu wa macho kama alivyo mwanae.

 Kwa upande wake katibu mtendaji wa shirikisho la chama cha watu wenye ulemavu manispaa ya Morogoro Nd.Athumani Ommary amesema bado kuna changamoto kwa jamii kukataa kuwaandisha watoto wenye ulemavu kwenye ofisi za chama cha watu wenye ulemavukupitia  kata husika kulingana na ulemavu alio nao.

Hata hivyo Elizabeth Julius amewaomba wazazi na walezi walio na watoto wenye ulemavu wa aina yeyote wasiwafiche ndani badala yake wakawaandikishe kwenye vyama vyao iliwapate huduma zinazo wastahili kulingana na maumbile yao, kwani kilammoja anahaki sawa yakuendelea kuishi kwa uhuru na kushiriki katika kuleta maendeleo yao na nchi kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments