Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

KAMUSI ELEKEZI NA WATOTO WENYE ULEMAVU.Mikataba mbali mbali ya nchi,afrika,dunia na ikiwemo kamusi elekezi ya watu wenye ulemavu ipo inayozungumzia kutoa kipaumbele,kusaidia  na kubaini  aina ya upofu na visababishi vinavyo sababisha mtu kupata ulemavu wa macho yaani upofu.

Kamusi Elekezi ya Ulemavu nchini uklasa wa 52-53 imeanza kwa kutofautisha aina ya kilema cha macho“Kilema cha uoni wa koteksi: aina ya kilema cha upofu ambacho husababishwa zaidi na matatizo ya ubongo kuliko yale ya jicho lenyewe. Visababishi hivi hupambanuliwa kwa majina, yaani kilema kinachotokana na hitilafu ya macho huitwa “cha uoni wa jicho” wakati kile kinachohusishwa na ubongo, huitwa cha koteksi”.

Inawezekana mtu kupatwa na aina zote mbili za vilema, yaani cha koteksi na cha jicho. Kilema cha uoni aina ya koteksi wakati mwingine huitwa upofu japo mtu mwenye kilema cha aina hii hawapotezi uoni kabisa. Dhana “kilema cha uoni wa kinyurolojia” hujumuisha aina zote mbili za upofu zilizozungumziwa awali.

Ukawiaji wa kukomaa kwa uoni ni aina nyingine ya kilema cha uoni wa koteksi ila chenyewe hujirekebisha katika kipindi cha miezi michache baada ya kuzaliwa. Japo kiwango cha uoni wa mtu mwenye aina hii ya kilema (cha uoni wa koteksi) kinaweza kubadilika, ni nadra sana (kama itatokea) kurekebika kabisa.

 Visababishi vikuu vya kilema cha uoni wa koteksi ni pamoja na: asfiksia, hipoksia au iskemia ambazo zinaweza kutokea wakati wa michakato ya kuzaliwa, uatilifu wa ukuaji wa ubongo, kujeruhika kichwani, hidrosifarasi, kiharusi kinachohusisha ndewe ya kisogoni, na maambukizo ya mfumo wa kati wa neva k.v. meninjitisi na ensefalitisi.

counseling: unasihi: utoaji elimu na ushauri kwa anayetatizwa na jambo kiasi cha yeye kushindwa kulipatia ufumbuzi. counselor: mnasihi: mtaalamu wa kutoa ushauri. covenant: mapatano: 1. ahadi ya kufanya au kutofanya jambo fulani maalumu; 2. kuingia katika mapatano rasmi (pia mkataba). 3. nadhiri ya maandishi ya siri ya kutoa malipo ya ufadhili kwa kipindi kilichopangwa.liii covenants on human rights: mapatano katika haki za binadamu”.

Aidha  kwa mjibu wa takwimu za Ofisi ya shirikisho la watu  wenye ulemavu manispaa ya Morogoro kupitia kwa katibu mtendaji Nd.Athumani Ommary zinaonyesha kuna watoto 88 wakiume 43 na wakike 45, hatahivyo akatoa rai kwa jamii kuhusu watoto walio na ulemavu wa macho kwa walio na tabia ya kuwa ficha na kutoa sababu zisizo za msingi ambazo zinasababisha kukwamisha utimizwaji wa haki zao za msingi zinazo wahusu watoto wenye ulemavu.

 Hata hivyo Willa Matika yeye ni mfamasia mkazi wa misufini manispaa ya Morogoro amesema jamii inapaswa kubadilika hususani namna ya kuwa tunza na kuwa hudumia watoto wenye ulemavu wa aina zote hasa maswala ya afya,wazazi na walezi wanapaswa kuwaandikisha watoto wao wenye ulemavu kwenye vitengo husika ilikuendelea kupata huduma za matibabu na mazoezi ikiwa hayo yote yanahitajika kwa mtoto husika kungali mapema,kwani kunaulemavu mwingine unaweza kupovywa kwa njia ya mazoezi akiwa bado mtoto mchanga.

Post a Comment

0 Comments