Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

Katibu tawala aagiza waajibishwe wazazi wasio changia chakula shuleni


Kufuatia kukithiri kwa tabia ya baadhi ya wazazi kugoma kabisa kuchangia uji na chakula shuleni kwa ajili ya watoto wao serikali mkoani Kagera imezitaka serikali za mitaa na vijiji kuunda sheria za kuwawajibisha wazazi hao ili wanafunzi waweze kuondokana na changamoto zinazowaata kutokana na kukosa huduma hiyo.

Katibu tawala wa mkoa huo Prof.Faustine Kamuzola amesema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa kikao cha ALAT mkoa na kwamba inasikitisha kuona yanakuweo makundi wakati wa utolewaji wa huduma ya uji shuleni (wanakula na wasiokula) na kwamba kwa asiyetoa inamuathiri kiasi kikubwa kwani humpunguzia uwezo wa kitaaluma.

Aidha amewaagiza wanasheria ofisi ya mkuu wa mkoa kuzisaidia serikali za mitaa kuunda hizo sheria ndogo na kuwasaidia katika michakato yote ya upitishaji ili izingatie utaratibu kisheria

Awali akiwasilisha taarifa kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa ALAT mkoa Bw,Kashunju Kanyuguli ameiomba serikali kuingilia kati utatuzi wa changamoto hiyo kwani wengi wao bado wanaamini kwamba serikali inatoa kila kitu kupitia elimu bure.

Kwa niaba ya wajumbe wa kikao hicho William Ruta amesema kuwa kuundwa kwa sheria hizo ndogo na iwapo zitatekelezwa kwa ufanisi mkubwa zitaleta matokeo chanya kwani wasio toa watawajibishwa na kama wazazi watatii sheria hizo mafanikio ya kitaaluma kwa wanafunzi yataongezeka.

Baadhi ya wazazi manispaa ya Bukoba wameiomba serikali ya mkoa huo kuendelea kuielimisha jamii  kuhusu utoafauti wa uchangiaji wa chakula shuleni na  elimu bure badala ya kujikita kwenye utungaji was Sheria za kuwabana wasio changia.Post a Comment

0 Comments