Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

KUFUNGWA KWA SHULE, SABABU YA UPUNGUFU WA DAMU SALAMA KAGERA.

                                                                          https://1.bp.blogspot.com/-bGEzos-W_rI/Xl52Zt5tdKI/AAAAAAAAAdI/FkJNb50iDIcQ7ln7eYjR4irKcc2ngAOqgCLcBGAsYHQ/s1600/DAMU%2BSALAMA..jpg

Kufungwa kwa shule na vyuo mkoani Kagera kumetajwa kupelekea changamoto ya upungufu wa damu salama kwenye benki ya damu kutokana na wanafunzi kuwa wadau wa kubwa wa uchangiaji damu.

Akizungumza na Kids Time/ UN Radio Mshauri na Msimamizi wa timu za ukusanyaji damu salama Mkoa, Amos Bashweka amesema, kasi ya utokaji wa damu kwenye benki hiyo ni kubwa ukilinganisha na inayoingia, kwani wanafunzi walikuwa na uwezo wa kutoa damu kwa wakati mmoja na kupatikana kwa wingi tofauti na sasa.

Aidha ameeleza kwamba, makundi makubwa yatakayoweza kuathirika katika upungufu huo wa damu katika benki ya damu salama ni wajawazito na watoto.

Kwa upande wake Mratibu wa kitengo cha damu salama mkoani Kagera, Mbakileki Audax amesema kuwa, Timu ya uhamasishaji na ukusanyaji damu huingia mtaani ili kuelimisha Umma.

"Ili kuhakikisha damu inapatikana ya kutosha na kunusuru maisha ya wahitaji, mwananchi kwa wakati afike kwenye kituo cha afya kuchangia damu na sio kwa mikusanyiko kufuatia kuwepo kwa tahadhari ya mikusanyiko" amesema.

Ignatio Haberi anayeuguliwa na mtoto katika hositali ya Rufaa ya Bukoba amewashauri wanatimu wa ukusanyaji damu salama, kufika vijijini kwani wapo watu ambao huguswa kuchangia damu lakini hukwama kutokana na umbali wa vituo vya Afya vilivyopo mjini.

Na, Rosemary Bundallah


Post a Comment

0 Comments