Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MABARAZA YA WATOTO HAYAKUWA ACHA NYUMA WATOTO WENYE ULEMAVU.
CRC nimkataba wenye haki zote ambazo watoto wote wanapaswa kuwa nazo,mkataba huu umetokana na Azimio la haki za binadamu baada ya ukatili uliofanyika kipindi cha vita kuu mbili ya dunia ya mwaka 1914-1918 na "Vita Kuu ya Pili ya Dunia" 1939-1945, kwa sababu hiyo kifungu cha tatu(3) aya ya kwanzan na yapili katika mkataba huu kinasema.

 “Kwa kutambua mahitaji maalum ya mtoto mlemavu, misaada iliyopitishwa kulingana na aya ya 2 ya kifungu cha sasa itatolewa bure, kila inapowezekana, kwa kuzingatia rasilimali za kifedha za wazazi au wengine wanaomtunza mtoto, na imeundwa ili kuhakikisha kuwa mtoto mlemavu ana uwezo wa kupata na kupokea elimu, mafunzo, huduma za afya, huduma za matunzo, maandalizi ya nafasi za ajira na burudani kwa njia inayofaa kumfanikisha mtoto kufikia ujumuishaji kamili wa kijamii na maendeleo ya mtu binafsi, pamoja na ukuaji wake wa kitamaduni na kiroho kisaikolojia na matibabu ya kazi ya watoto walemavu”.

Kufuatia mkataba huu wa haki za watoto duniani TKT/UN Radio ili lazimika kuwatafuta viongozi wa mabaraza ya watoto Tanzania bara na Visiwani ilikufahamu zaidi wanavyo shirikiana  na  watu wenye ulemavu kwenye mabaraza yao.

Asia Makame ni mwenyekiti wa baraza la watoto Zanzibar nilizungumza nae kwa njia ya simu kuhusu ushirikiano wa viongozi wa mabaraza wanavyo shirikiana na watu wenye ulemavukatika majukumu yao “Niliona kwamba ili nifanye kazi nzuri nilazima nizingatie haki na usawa kwa makundi yote,  kuna watoto wenye mahitaji maalumu watatu(3) mmoja ana umri wa miaka minne nimlemavu wa mguu,mmoja anamiaka sita ambae nimlemavu wa macho na watatu ni mwenye ualbino”.

Kwa upande wa Tanzania bara nime zungumza na baadhi ya viongozi na wajumbe wa baraza la watoto,Mkoa wa Morogoro,Shinyanga na Songwe, kutoka mkoa wa Shinyanga nimezngumza na katibu wa baraza la watoto mkoani humo Nd.Sospeter Lemgoha amesema “ Kazi kubwa tunazo zifanya nikuhakikisha tunajenga ustawi wa mtoto,kutoa elimu dhidi ya kutambua haki na wajibu wa watoto kujitolea kwenye jamii kwa kama vile kufanya usafi wa maeneo ya ofisi za serikali”

Aidha Lemgoha amebainisha kuhusu fursa za uongozi kwa watoto wenye ulemavu katika baraza hilo kua kuna mtoto mmoja mwenye ualbino ambae yeye ni mjumbe wa baraza kwa ngazi ya mkoa, na akataja maeneo yalio kithili kwa matukio ya ukatili wa mimba,ndoa na ajira za utotoni, inayo ongoza kwa mjibu wa taarifa za mwaka 2019 ni Wilaya ya Kishapu.


Kutoka mkoani Morogoro nimezngumza na mwenyekiti msaidizi Paulina Anols wa baraza la watoto  Manispaa ya Morogoro, ambapo amesema katika baraza lao hakuna kiongozi mwenye ulemavu isipokuwa kupitia kata ishirini na (29) za Manispaa kuna washirika wa kutoka  makundindi yote ya watu wenye ulemavu.

Hata hivyo mwenyekiti wa baraza la watoto mkoa wa Songwe Lilian Shayo amesema changamoto kubwa wanayo kumbana nayo katika kutekeleza majukumu yao ni kwa baadhi ya wazazi na watoto hushindwa kutoa ushirikiano wakupata taarifa sahihi za msingi kunapo kuwa na matukio ya ukatili dhidi ya watoto, nakuomba serikali na wadau mbali mbali kuendelea kuunga mkono mabaraza ya watoto nchini hasa watoto wenye mahitaji maalumu wanapo peleka maombi ya mahitaji yao kwa utaratibu unao kubalika kwenye ofisi za serikali na binafsi.Post a Comment

0 Comments