Advertisement

Responsive Advertisement

Navigation Menu

MOWECS YATOA RIPOTI YAKE YA WATOTO WENYE ULEMAVU MOROGORO.


MOWECS
Shirika la  MOWECS limetoa ripoti yake ya awali iliofanyika mwaka jana 2019 ilio husu watoto wenye ulemavu wanao ishi katika mazingira hatarishi ndani ya  manispaa ya Morogoro.
Shirika lisilo la kiserikali la Morogoro Organization for Women,Elders and Child Support (MOWECS) lenye makao mkuu yake mkundi mkoani Morogoro linalo jihusisha na kusaidia wanawake,wazee na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapatia elimu ya kiuchumi iliwaweze kuanzisha biashara/kazi zitakazo wapatia mahitaji muhimu ya kilasiku, kamavile chakula,mavazi namalazi,na mahitaji ya kijamii kamavile Elimu,Afya,Mazingira na miundo mbinu rafiki kwa watoto wenye ulemavu.

Akisoma ripoti hiyo mkurungenzi mtendaji wa shilrika hilo Bi,Marry Mafwimbo amesema wapo walemavu kutoka kata tatu zilizopo manispaa ya Morogoro ambazo ni chamwino,Lukobe na Mkundi ambao wanauhitaji tofauti tofauti kamavile baiskeli za miguu  mitatu(wheelchair),mavazi,lishe bora,bima za afya,maradhi na mahitaji mengine ya msingi kulingana na hali ya mtoto,aidha kuna watoto ambao shirika linamalengo ya kuwapeleka katikavyuo vya ufundi ili waweze kuji kwamua kutoka katika halingumu ya maisha wanayopitia.

  Aidha utafiti huo ulifanikiwa kubaini walemavu wapatao kumi natano(15)ambao miongoni mwao niwalemavu wa ngozi, akili na viungo wanaoishi katika mazingira hatarishi. 
MOWECS
 Hata hivyo utafiti ulikuwa na lengo la kubaini watoto wenye mahitaji maalumu ,nakuona namna watakavyo ziwezesha familia zao kwa kuunda vikundi vya kiuchu ilikuongeza kipato cha familia na kuwa nauhakika wa kupa mahitaji ya kilasiku yakiwemo Afya,Elimu,Lishe bora,Mazingira na Miundo mbinu rafiki na Ukuwaji wa Uchumi.

  Kwa upande mwingine bi,Marry akafafanua zaidi kwa watoto wenye ulemavu wa utindio wa ubongo, amesema watoto wa aina hiyo wana hitaji lishe bora, itakayo wa wezesha kuongeza na kuimarisha kinga zao za mwili na mavazi yanayo wasaidia wakati wakujisaidia yaani pampas kwa,upande wamaliwato.

Post a Comment

0 Comments